Habari

Muimbaji Boaz Danken Kuzindua Album Mbili Mwezi wa 8 Jijini Mwanza

Mwimbaji wa nyimbo za injili Boaz Danken kutoka jijini mwanza anatarajia kufanya uzinduzi wa matoleo yake mawili ya albamu mapema tarehe 6 ya mwezi wa nane mwaka huu wa 2017 katika ukumbi wa hotel ya Gold Crest jijini mwanza.

Matoleo ya album hizo yanakwenda kwa jina la Haufananishi na Emmanuel yote yakiwa yamerekodiwa live.

Boaz ni miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania wanaofanya recording za album zao live na ikumbukwe tu mwaka jana kwenye miezi ya mwishoni mwishoni hivi alifanya recording ya matoleo ambayo yatazinduliwa rasmi mwezi ujao.

 

Pamoja na yeye waimbaji wengine toka ndani na nje ya jiji la mwanza watakuwepo kuhudumu nae akiwemo Jay Johnas toka jijini Arusha, Eliya Andendekisye Mwantondo toka Arusha, Joel Kaema, Misericordias Mushi na wengine wengi watakuwepo.

Misericordias Mushi atahudumu na saxophone

Boaz anachukua nafasi hii kukukaribisha mtu wa Mungu katika ibada ya uzinduzi wake huo wa album zake hizo ambapo viingilio kwa viti vya kawaida itakuwa ni shilingi elfu kumi na kwa viti maalum V.I.P ni shilingi elfu ishirini.

Elia nae atahudumu

Boaz ameandika haya kupitia ukurasa wake wa facebook kupitia uzinduzi wake anaotarajia kuufanya tarehe 6 ya mwezi wa 8 naona Urejesho wa utukufu wa Mungu Tena waliokata tamaa Wanatiwa Moyo tena
– Waliokuwa na majeraha Yesu Anayatibu kabisa
– Wasiompokea Yesu wanamwamini Yesu Kuwa Bwana na mwokozi wa maisha Yao
Yesu anafanya kazi ya uponyaji mpaka sasa
– Wafu wanafufuka mpaka sasa kwa jina la Yesu kristo

-YALIYOSHINDIKANA KWA WANADAM KWA MUNGU YANAWEZEKANA

#ANAFANYA MAMBO AMBAYO MWANADAMU HAWEZI KUFANYA.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Ibitayo Jeje - Mama mi

Next post

Habari Picha za Tamasha la Wanawake Waombolezao Kitaifa 20.07.2017. Hizi Hapa.