Habari

Msimu Wa Pili Wa Tamasha La Siku Ya Sifa Arusha Kuanza March 12 Mwaka Huu.

Baada ya kimya cha muda sasa ibada Tamasha la Siku Ya Sifa linalofanyika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania hatimaye msimu wa pili wa Tamsha hilo unatarajiwa kuanza tarehe 12 ya mwezi huu wa tatu.

Taarifa rasmi za kuanza kwa Tamsha hili GospoMedia umezipata kupitia kipindi cha Radio Cha Praise Time kinachoruka kupitia Habari maalum Fm Arusha.

GospoMedia imefanya mahojiano na waandaaji wa Tamsha hilo ambao ni Habari Maalum Media kupitia Radio yao ya Habari Maalum Fm na kusema kuwa baada ya kumalizika kwa msimu wa tamasha hilo mwaka jana mwezi wa 10 sasa mwaka huu wanaanza msimu wa pili kwa nguvu kubwa na kuamini ya kuwa mwaka huu itakuwa zaidi ya mwaka jana.

“tunamshukuru Mungu mwaka jana tulifanya msimu wa kwanza ikiwa ni mara ya kwanza kuitambulisha siku ya sifa na tunaamini mwaka huu itakuwa na utukufu zaidi ya ule wa mwaka jana”

Waandaaji hao wameeleza kuwa Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 12 ya mwezi wa tatu katikati ya jiji la Arusha katika ukumbi wa Lunch Hour kwa Pastor Chuma karibu na ukumbi wa metropole Hall nyuma ya bank ya NBC arusha.

Wameeleza kuwa lengo la Tamsha hili ni kuwaleta watu pamoja kwaajiri ya kumsifu Mungu katika utakatifu.

Waimbaji wanaotarajiwa kushiriki na kuhudumu katika siku hiyo ni pamoja na waimbaji Saimon Rweikiza ambaye atashiriki kwa mara ya kwanza pamoja na mwimbaji mwingine ambae mwaka huu ndio ameanza na kazi yake imepokelewa vizuri anaitwa Alicia Charles wakishirikiana na waimbaji wengine kama Mnene Makweta  sasa hivi Maarufu kama baba Diva ,Shadrack Robert, Solomon Mudogo, B Zabron Senior, God-Surrender’s, Nestory Ihano,  Esther Yohana, Jenipher Sitta pamoja na kundi la kusifu na kuabudu la Rhema Worship .

Habari maalum Fm inakukaribisha wewe mkazi wa Arusha kushiriki katika tamasha hilo siku ya jumapili ya tarehe 12 pale Lunch Hour kwa Pastor Chuma.

Kauli mbiu ya msimu huu wa pili wa tamasha la siku ya sifa ni

#TwenzetuSikuYaSifaMarch12

GospoMedia itakuwa karibu kuendelea kukupa taarifa wewe mkazi wa Arusha na viunga vyake.

Advertisements
Previous post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Ephraim Ezekiel-Mkono wa Mungu

Next post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Josiah Justice - Ni Wewe Uliyetenda