Habari

Mshindi Wa Nne Wa Gss Kaskazini Saimon Rweikiza Kuzindua Album Ya Mbarikiwa Jijini Arusha.

Mwimbaji wa nyimbo za injili anayefanya vizuri kwa sasa jijini Arusha Saimon Rweikiza anatarajia kuzindua album yake ya kwanza aliyoipa jina la MBARIKIWA.

Akizungumza na GospoMedia jijini Arusha saimon amesema anatarajia kufanya uzinduzi wa album yake tarehe 30 ya mwezi wan ne katika jiji la Arusha katika kanisa la PEFA MLIMA WA BWANA sakina matejoo.

Saimon ambaye mwaka jana alishiriki mashindano ya kusaka waimbaji wa nyimbo za injili ukanda wa kaskaini na kushika nafasi ya nne ameiambia GospoMedia kuwa anamshukuru Mungu sababu amekamilisha album yenye nyimbo saba na yuko tayari kwaajili ya uzinduzi .

Saimon akihudumu kwenye moja ya ibada aliyoalikwa

Saimon amesema mbali na uimbaji yeye ni mhitimu wa shahada ya elimu katika chuo kikuu cha arusha lakini pia ni mwalimu wa uimbaji,step master, MC, DJ na vipawa vingine vingi ambavyo Mungu ameweka ndani yake.

Mwimbaji huyo amewashukuru familia yake kwa kumtia moyo na kumsapoti kwa kila jambo lakini pia kituo cha radio cha habari maalum fm arusha 97.7 ambapo ndio wasaidia pia kumtamburisha kwa watu wengi zaidi.

Saimon kwenye jukwaaa la GSS Arusha

Aidha ameongeza kuwa anashukuru shirika la YSSM chini ya Mkurugenzi wake ndugu Elihuruma Maruma kwa sapoti yao pia na studio aliofanyia kazi chini ya producer Elisha.

Saimon ameweka wazi kuwa lengo la kufanya uzinduzi huo ni kwaajiri ya kukusanya fedha kwaajiri ya kusaidia kufanya album ya video ambayo anatarajia pia kuiachia mwaka huu.

Saimon anawakaribisha watu wote katika uzinduzi huo ambao anaamini pia utabadirisha maisha yako.

Unaweza kuwasiliana na muimbaji Saimon Rweikiza kupitia +255653624729 au +255768221353
Facebook: Saimon Rweikiza
Instagram: @saimon_rweikiza
Twitter: @saimonrweikiza

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Sikiliza & Download Official GospeMusic Audio: Iman Victor-Unijaze

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Pastor Eric Hance Mtalemwa-Nauona Muujiza