Habari

Mshindi Wa GSS Kaskazini Kelvin Weber Auelezea Wimbo Wake Unavyogusa.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Kelvini Weber ambaye mwishoni mwa mwaka 2016 alishinda taji la mshindi wa mashindano ya waimbaji wa nyimbo za injili kwa upande wa ukanda wa kaskazini uliojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara amezungumzia wimbo wake wa kwanza aliouachia mapema mwaka huu unavyogusa maisha yake binafsi na watu wengine.

Akizungumza kwenye kipindi cha Praise Time ya Habari Maalum Fm Arusha kwenye kipengele cha Gospel News Weber amewashukuru wasikilizaji kwa wimbo wake kuwa wimbo bora wa wiki.

Weber ameeleza wakati anaandika wimbo wa Nitumie anaeleza alikuwa katika mazingira tulivu ambayo alikuwa akihitaji Mungu amtumie sio kwenye uimbaji tu lakini katika kila jambo analolifanya.

“ninatamani Mungu anitumie kwenye kila ninachokifanya sio uimbaji tu lakini biashara zangu, kupenda kwangu kuishi kwangu na kila minachokifanya Mungu aonekane na watu wamtukuze yeye katika hilo”

Weber ameeleza kuwa siku moja alikuwa kwenye mkutano wa injili alikuwa anapiga gitaa la bass na kuna mtu aliokoka kupitia mkutano huo na kushuhudia kuwa alisikia Mungu akizungumza nae kupitia gitaa la bass.
Weber amewataka watu kumuomba Mungu awatumie kwenye mambo wanayoyafanya kwasababu Mungu hajawaweka watu mahali kwa bahati mbaya.

Tayari Weber ameshafanya video ya Wimbo huo wa nitumie na muda wowote anaweza kuiachia lakini pia amesema yuko mbioni kutoa wimbo mwingine ambao anaamini wimbo huo utawahudumia watu pia.

GospoMedia itaendelea kukupa habari kuhusiana na ujio wa kazi zake hizo ambazo anatarajia kuziachia hivi karibuni.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Hezekiah Rubete-Uliponitoa Ni Mbali

Next post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Mc Freddie Feat Mr.Mike-Wakusamehe