Connect with us

Music Video | Audio: Mr.Seed Feat Size 8 – Simba wa Yudah

Muziki

Music Video | Audio: Mr.Seed Feat Size 8 – Simba wa Yudah

Kutoka jijini Nairobi leo kwa mara nyingine tena nimekuwekea video nzuri iitwayo Simba wa Yudah kutoka kwa moja ya mwimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Kenya anayefahamika kwa jina la Mr.Seed hapa akiwa amemshirikisha mwimbaji mahiri aliyefanikiwa kupata tuzo kadhaa nchini humo anayefahamika kwa jina la Size 8.

Video hii imeongozwa na director Rahim na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za EMB records chini ya mikono ya prodyuza Paulo.

Simba wa Yudah ni wimbo wa sifa na ushuhuda ukieleza jinsi nguvu ya Yesu Kristo inavyotenda miujiza kwa watu na kubadilisha maisha kutoka dhambini na kurudi mahali patakatifu, kupitia wimbo huu pia Mr.Seed anadhihirisha kuwa hata yeye kuwa hapo alipo ni kwasababu Simba wa Yudah aliunguruma kwake na kusababisha maisha yake kubadilika kabisa.

Hata wewe ambaye kwasasa unapitia changamoto na matatizo kila kona kupitia wimbo huu unahimizwa kumwamini Yesu Kristo ili aweze kubadilisha maisha yako leo. ”Simba wa Yuda anaunguruma…na akiunguruma watu wanaokoka…”

Naamini utafurahia video hii na wimbo huu ambao ni hakika utatenda jambo ndani ya moyo wako leo, Naomba uchukue dakika zako chache kutazama video hii naamini utabarikiwa….

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na muimbaji Mr.seed kupitia:
Facebook Page: Mr Seed
Instagram: @mrseedofficial
Youtube: Mr.seedOfficial Music

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top