Habari

Mkurugenzi wa DAWASA aahidi kugharamia kolabo ya Mwamini Muyero na Ambwene Mwasongwe.

Mkurugenzi wa DAWASA, Bw.Charles Makoya ameahidi kugharamia kolabo ya waimbaji Mwamini Muyero na Ambwene Mwasongwe.

Bw. Makoya ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa album ya mwimbaji Mwamini Muyero kwa niaba ya waziri wa maji alitoa ahadi hiyo jumapili iliyopita katika kanisa la C.A.G Ubungo ambapo uzinduzi huo ulikuwa ukifanyika.

Katika kumsapoti Mwamini Bw. Makoya kwa niaba ya Waziri wa Maji Mh.Lwenje alichangia milioni mbili na kununua DVD ya Mwamini kwa shilingi milioni moja na kumwomba Ambwene Mwasongwe ambaye alikuwa moja ya waimbaji waalikwa kufanya kolabo na Mwamini ambayo yeye ataigharamia akisisitiza kuwa anataka aisimamie iwe na viwango vikubwa.

Kujua zaidi aliichoongea Tazama kwenye video tuliyokuwekea..

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Music Audio: Gideon Mussa-Africa

Next post

Download Music Audio+Video: Eunice Mtavangu-Nafsi Yangu