Connect with us

Music Audio: Miriam Jackson Feat Joshua Mlelwa – Nisaidie

Audio

Music Audio: Miriam Jackson Feat Joshua Mlelwa – Nisaidie

Kutoka jijini Dar es salaam leo nimekuletea wimbo wenye ujumbe wa matumaini uitwao Nisaidie kutoka kwa muimbaji Miriam Jackson akiwa na muimbaji mahiri na mkongwe anayefahamika kwa jina la Joshua Mlelwa, muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za Shekinah.

Akizungumzia kuhusu wimbo huu mwimbaji Miriam Jackson alikuwa na ujumbe huu:-

”Unajua katika hii nchi yetu au dunia hii watu wengi wanadhani shida, masimango, visa na hata maneno yatadumu pasipo kujua yatakoma. Naomba ni kushuhudie jambo moja… Leo wanavyokutazama tena na kusema kikowapi 2017 mbona aolewi, mbona afanikiwi, mbona sijui hivi na vile… Yani wanaongea mpaka inafika mahali hutaki kuwa na rafiki kwamaana unadhani matatizo, dhiki ulizaliwa nazo. Leo kupitia wimbo huu nakutangazia matataizo yako yatakoma.”

Hata hivyo Miriam Jackson amesema kuwa video ya wimbo huu ipo mbioni kutoka ikiwa imeongozwa na moja ya madirector wanaofanya vyema kwasasa akifahamika kwa jina la Msafiri kutoka Kwetu studio.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na Miriam Jackson kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 784 323 036
Facebook: Miriam Jackson
Instagram: @miriamjackson_tz

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Audio

To Top