Video

Video | Audio: Mike & Deglorious – Jesus

Kutoka nchini nigeria leo nimekusogezea video na wimbo mzuri wa kuabudu kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa injili nchini humo akifahamika kwa jina la Mike akishirikiana na kikundi cha nyimbo za sifa kijulikanacho kwa jina la Deglorious.

”Biblia inasema: Niite siku za shida zako nami nitakusikia”. Ninakutaka wewe kuita jina la Yesu leo ​na utaona jinsi ambavyo Yesu atakavyogeuza hali iliyo mbaya katika maisha yako na kuwa ushuhuda, Endelea kuamini katika jina la Yesu Ameen.” –  Mike

”Kuna kitu katika jina hili la Yesu
Jina hili linaweza kuponya Moyo uliovunjika
Hivyo tunapoita jina la Yesu
Kila hofu na dhoruba zitakoma
Kila hofu na dhoruba zitakoma.”

”Anakupa furaha, huondoa aibu.
Na anakufanya uwe mpya
Hivyo tunapoita jina la Yesu
Unachoomba ndio kile atakachokupa
Tunachoomba ni hakika tutapata” – Haya ni baadhi ya mashairi yanayopatikana katika wimbo huu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ikiwa ni moja kati ya nyimbo yenye mguso wa kipekee sana itakayobadilisha maisha katika mwaka 2018 nina imani kupitia jina la Yesu utainuliwa na kukalishwa mahali pa juu. Barikiwa!

Download Audio

Social Media
Facebook: De Glorious
Instagram: @degloriousministers
Twitter: @degloriousmin
Email: deglorious4real@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Elder Dempster – Only You

Next post

Audio: Chi-Gospel – Ebighi Ebi (Everlasting God)