Habari

Mchungaji aliyejaribu kumfufua mfu akamatwa Msumbiji

Mchungaji mmoja nchini Msumbiji amejikuta yupo mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio.

Mchungaji huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia asafiri hadi katika hospitali ya Chimoio katika jimbo la Manica, kufanya muujiza huo. Mchungaji huyo ambaye aliyedai kuwa na uwezo wa kufanya muujiza huo aliweza kuikonga mioyo ya maafisa wa hospitali hadi wakamruhusu aingie ndani ya chumba cha maiti kutekeleza muujiza wake.

Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi makali, hakuweza kabisa kurejesha uhai wa marehemu, Haikuishangaza familia ya marehemu.

Dada yake marehemu – ambaye hakutaka jina lake litajwe – aliwaambia waandishi wa habari:

“Mchungaji aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba. Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja mchungaji alipaza sauti akisema: ‘amka, kijana wa Mungu!”

“Hatukuamini mchungaji angefanya muujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.

“Tangu wakati huo mchungaji huyo alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu.”

Chanzo: BBC Swahili

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Papa Francis apingwa na kutetewa baada ya kusema kuzimu haipo

Next post

Audio: Faraja Hannington - Wingu