Ndoa na Familia

MFAHAMU INDIRA GANDHI WAZIRI MKUU WA KWANZA MWANAMKE INDIA.

Indira Gandhi alikuwa waziri mkuu wa tatu, alitumikia kiti hicho mnamo mwaka 1966 mpaka 1984, ambapo ulikuwa ni mwisho wa maisha yake kwa kuuwawa. Alikuwa mtoto wa Jawahrlal Nehru, Waziri mkuu wa kwanza wa India.
Indira Gandhi alizaliwa Novemba 19 mwana 1917, Allahabad, India. Gandhi alizaliwa katika familia iliyokuwa yajihusisha na siasa ya  Nehru; baba yake Jawaharlal Nehru, alikuwa waziri  mkuu wa nchi ya India. Gandhi alitumikia kiti cha uwaziri mkuu kwa miongo mitatu, kati ya mwaka 1966 mpaka 1977, na kipindi kiingine kilianza 1980. Mwaka 1984, Gandhi aliuawa na mlinzi wake wa dini ya Shikh.
Indira Gandhi alikuwa ni mtoto wa pekee kwa Jawaharlal Nehru na pia waziri mkuu wa kwanza baada ya India kujitegemea yenyewe. Indira alikuwa mchangamfu na alifurahia elimu katika shule za Kiswizi (Swiss)  na Chuo cha  Smorville, Oxford.
INDIRA GANDHI1
Baada ya mama yake kufariki mwana 1936, Gandhi alimtunza Baba yake, na kujifunza mahusiano ya kidiplomasia na viongozi wakubwa duniani kwa wakati huo.
Miaka ya 1980, kundi la dini ya Shikh lilikuzwa India, ambapo Gandhi alijaribu kulitawanyisha. Shikh wenye msimamo mkali walifanya kampeni katika Hekalu la dhahabu na Gandhi akaagiza askari 70,000 kuvunja hekalu takatifu. Zaidi ya watu 450 walikufa.
Mwezi Oktoba 31 mwaka 1984, mlinzi wa Gandhi aliyeaminika, aliyekuwa ni Mshikh, alitoa bastola na kumpiga Gandhi bila kusita. Na mlinzi mwingine, naye Mshikh, akachukua bastola automatic akampiga mara 38 mwilini mwake. Gandhi alifariki akipelekwa hospitali.
Indira Gadhi ndiye Mwanamke wa kwanza kushika ngazi ya juu India, na ni Waziri wa pili kuongoza kwa muda mrefu zaidi.
Indira Gandhi
Alipendwa sana na wananchi kwa ushujaa wake na kuwafukuza kazi waliokuwa vigogo na kukuza kilimo ambacho kilisaidia wananchi wengi wa hali ya chini.
Mtoto pekee kwa waziri mkuu wa kwanza naye kuwa waziri, somo kubwa katika habari ni kwamba wazazi tuna nafasi kubwa sana ya kuwafanya watoto wetu kufika tunapotaka kuwaona wamefika, Wasaidie wanao kuwa na marafiki wataowasaidia, wakutanishe na watu watakao watia changamoto, watapata nafasi ya kufahamu wanataka kuwa akina nani.Kuna kitu dunia kinasubiri kutoka kwa mwanamke fulani, kijana fulani, tusipofanya hivyo tunawapotezea malengo.
Douglas Kyungai a.k.a Dolaa
GospoMedia Reporter Arusha zone
+255767844858
Dolaa

Dolaa

Douglas Kyungai(Dolaa) Chief Photographer & Production Manager wa GOSPOMEDIA.

Previous post

DOWNLOAD WIMBO MPYA KUTOKA KWA ELLYTHOMAS-TAMANIO LANGU

Next post

HAPPY BIRTHDAY GOSPOMEDIA.COM KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA