Video | Audio: Method Mathew - Mbele Yangu - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Method Mathew – Mbele Yangu

Video

Video | Audio: Method Mathew – Mbele Yangu

Kutoka jijini Arusha leo tumekusogezea video ya wimbo mzuri unaokwenda kwa jina la Mbele Yangu kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayefahamika kwa jina Method Mathew, Video hii inabeba jina la albamu yake ya DVD ikiwa imeongozwa na BSM Production, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Boaz Silas.

“Lengo la wimbo huu ni kuwakumbusha na kuwahimiza watu wajiamini wanapofanya jambo lolote jema na lenye kumtukuza Mungu huku wakiwa na mtazamo chanya wa kuona mafanikio mbele yao na kutokata tamaa pale wanapopitia shida kwani shida zinapozidi ushindi unakuwa umekaribia. Watu waamini kuwa vinywa vyao vina nguvu ya kuumba ambapo kama wakivitumia vizuri kwa kujitamkia na kujiumbia mambo mazuri yatakuwa kama yalivyo tamkwa mwisho watu wa Mungu wasitishwe na maadui kwani watakuja kwa njia moja Mungu atawatawanya kwa njia saba wazidi kuona mema mbele yao siku zote.” – alisema Method Mathew

Hakika huu ni moja kati ya nyimbo nzuri ambayo hutakiwi kuacha kusikiliza kila wakati, Huu ni wimbo ambao utakufanya uwe mtu mpya kila siku kwa maana umejaa nguvu ya kukupa mtazamo mpya utaokuwezesha kushinda vita zote mbele yako huku ukimtegemea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika utabarikiwa kila siku, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi, mialiko ya kihuduma na jinsi ya kuipata nakala ya albamu yake wasiliana na mwimbaji Method Mathew kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 766 53 2181
Facebook: Method Mathew
Instagram: @method_mathew
Youtube: Method mathew

1 Comment

1 Comment

  1. kisulasaimon

    January 7, 2019 at 9:45 pm

    Mungu akubariki @method mathew

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top