Videos

Music Video | Audio: Mercy Masika – Upendo

Kwa mara nyingine tena kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mercy Masika wa jijini Nairobi ametuletea zawadi nyingine ya video ya wimbo wake mzuri na wenye kubariki mno uitwao Upendo, video na wimbo huu vyote vikiwa vimefanyika chini ya usimamizi wa studio za Still Alive Production zilizopo nchini kenya.

Upendo ni wimbo na video ya sifa ambayo muimbaji Mery masika aliachia siku ya Krismasi ikiwa ni zawadi maalumu kwa watu wote katika kusherehekea siku hiyo Takatifu na kuwakumbusha watu maana halisi ya upendo ambao asili yake ni Mungu mwenyewe ambaye aliupenda ulimwengu na akamtoa mwana wake wa pekee Yesu Kristo aje kutukomboa ili mimi na wewe tuwe huru na kuwa mbali na dhambi.

Katika wimbo huu pia mtumishi wa Mungu Mercy Masika amezungungumzia juu ya suala la kumshukuru Mungu kwa kututunza na kutulinda kwa kipindi chote cha mwaka mzima hadi sasa tunapoeleka kumaliza mwaka upendo wa Yesu umekuwa nasi na kutudhihirishia ushindi wa kutuvusha mwaka mwingine.

”Kubalikiwa sio mali ni kunyenyekea na kumpata Yesu….” moja kati ya mistari inayopatikana kwenye wimbo huu mzuri uliobeba ujumbe wa neno la Mungu ambalo naamini litakwenda kubadilisha maisha yako siku ya leo na upendo wa Yesu ukatawale maisha yako…

Umempata Yesu sema Yeah Yeah …. Umempata Yesu sema Yeah Yeah……Amekuokoa sema Yeah Yeah….

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina amini utakubariki siku zote. Karibu uinuliwe!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na muimbaji Mercy Masika kupitia:
Facebook Page: Mercy Masika
Instagram: @mercymasika
Youtube: Mercy Masika

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Audio: Liza J - Nakupenda Pia

Next post

Music Audio: Ibek Caleb – Something About You God