Habari

Mchungaji ahukumiwa miaka saba jela kwa kuvuka mipaka nchi kinyume cha sheria

Na mwandishi wetu,

Mchungaji mmoja raia wa Marekani akifahamika kwa jina la John Cao mwenye asili ya China amehukumiwa miaka saba gerezani na kutozwa faini kubwa ya pesa baada ya kudaiwa kupanga mipango ya kuvuka mipaka ya nchi hiyo kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taasisi ya watetezi wa wakristo na misaada nchini china (Persecution Watchdog China Aid), imesema mahakama ya jimbo la kusini mwa mji wa Yunnan nchini China ilitoa hukumu hiyo Machi 23, mwaka mmoja baada ya Mchungaji John Cao kushikwa na hatia ya kujihusisha na utoaji wa misaada kando kando ya mpaka wa China-Burma.

Maofisa hao walimshutumu Cao na mfanyakazi mwenzake, Mkristo aitwaye Jing Ruxia, kwa kupanga mipango ya kuvuka moja ya mipaka ya nchi hiyo kinyume cha sheria, ingawa wamekuwa wakifanya hivyo mara nyingi kabla hawajakabiliwa na mashtaka hayo.

Mchungaji John Cao, anaheshimiwa sana kwa mchango wake katika jamii nchini humo kwa kujenga shule 16 ambazo zinawasaidia watoto zaidi ya 2,000 wenye uhitaji wa elimu katika mji wa kaskazini mwa Myanmar, hukumu hiyo inawalazimisha kutumikia kifungo cha miaka saba na kulipa faini ya Yuan 20,000 za china ambayo ni sawa na dola za 3,000 za marekani.

Jing, ambaye aliwahi kuachiwa huru baada ya kutumikia kifungo mwaka mmoja gerezani, kwa mara nyingine tena alipata hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja na faini ya Yuan 5,000 za china ambayo ni sawa na takribani dola 792 za marekani.

Mchungaji John Cao ambaye makao yake ya kudumu yapo nchini marekani tangu 1990 lakini aliendelea kuwa raia wa China ili apate kibali cha kuingia nchini humo kwa ajili ya kazi yake ya utume na utoaji wa misaada. Cao pia aliwahi kuchunga kanisa liitwalo Greensboro, lililopo jijini New York, Marekani, ambapo baadae alioa raia wa marekani na kubarikiwa kupata watoto wawili, ambao bado wanaishi nchini Marekani.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mc Freddie afunga ndoa Ghafla

Next post

Wadau wagusia mambo sita ya waraka wa KKKT