Connect with us

Mc Freddie afunga ndoa Ghafla

Habari

Mc Freddie afunga ndoa Ghafla

Na mwandishi wetu, Morogoro.

Rapa wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Mc Freddie ameweka wazi juu ya kuingia rasmi kwenye taasisi ya ndoa baada ya kufunga ndoa na mke wake aitwaye Mariam Alphonse jumatatu ya tarehe 27.03.2018.

Akiongea na gospomedia.com Mc Freddie ambaye kwa jina kamili akifahamika kama Fredrick Timothy alikuwa na haya ya kusema:-

”Napenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki katika kuhakikisha harusi yangu imekwenda sawa. Binafsi sina cha kuwalipa zaidi ya shukrani. Japokuwa ilikua ghafla sana ila Kwa support mlioionyesha kwa kweli sikutegemea mimi na mke wangu tumefurahi sana. Mungu awabariki.” – Alisema Mc Freddie

Kwa mujibu wa Mc Freddie alisema harusi hiyo ilifungwa katika kanisa la kibatist mkoani Morogoro chini ya mchungaji Samwel Denis ambaye ndiye aliyefungisha ndoa hiyo na kuwapa Baraka zote za ndoa yao.

Mc Freddie ni rapa ambaye amepata kutambulika katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania kupitia nyimbo zake kadhaa ikiwemo Wakusamehe, Kanisani na Siteketei ambazo kwa hakika zimemtambulisha vyema na kupokelewa vizuri.

Kwa niaba ya uongozi wa gospo media tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Mc Freddie kwa hatua kubwa aliyopiga katika maisha yake, tunaamini Mungu ataitunza na kuilinda ndoa yake, Ameen.

Kama bado hujawahi kutazama video yake iitwayo Sitetekei akiwa amemshirikisha Juliana aliyoiachia mwaka 2017, nakukaribisha sasa uweze kubarikiwa kwa kuitazama video hii na kupakua wimbo huu iwe zawadi kwako siku ya leo, ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Mc Freddie kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 654 051 919
Facebook: Fredie Mc
Instagram: @mc_freddie_believer

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Habari

To Top