Habari

MASHAIRI YA WIMBO WA JENIPHER SITTA, UPO NA MIMI YAKO HAPA

Verse 1

Nilipokata tamaa, ulinitia moyo,

Nilipokosa nguvu, ulinitia nguvu,

Nilipokosa tumaini, ulinipa tumaini,

Nilipokuwa na majonzi, ulinipa faraja,

Nilipokuwa nimetengwa,wewe ulinikumbatia.

Chorus

Ulikuwa na mimi, hata leo upo na mimi,najua upo na mimi hautaniacha kamwe.

Verse 2

Wewe Bwana nimekufanya,faraja ya moyo wangu,

Wewe kipenzi cha moyo wangu,wakati wote maishani mwangu,

Wewe ndiwe mwanga,wa njia zangu,

Usiniache nimekutumainia wewe pekee.

Chorus

Ulikuwa na mimi,hata leo upo na mimi,najua upo na mimi, hautaniacha kamwe.

Bridge

Wewe ni rafiki yangu, wa pekee sana maishani mwangu,

Hakuna kama wewe, mmh!

Haulinganishwi na chochote,duniani na mbinguni pote, wewe ni alpha na omega, mmh!

Kabla sijaumbwa tumboni, ulinijua na kunitakasa, na ulikuwa na mimi, iii!

Hata leo watenda kazi na mimi,

Hata leo watembea na mimi,

Hata kuimba waimba na mimi,

Na upo na mimiiiii

Heeeeeee

Chorus

Ulikuwa na mimi, hata leo upo na mimi,najua upo na mimi hautaniacha kamwe

Unaweza kusikiliza na kupakua wimbo wa Jenipher Sitta  Upo na Mimi kwa kubonyeza HAPA

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

HIVI NDIVYO MHARIRI WA BONGO 5 ALIVYOIFAGILIA ALBUM YA ANGEL BENARD.

Next post

TAZAMA LIVE PERFOMANCE YA UNCLE EMMA AKIIMBA NAFURAHI, ARUSHA.