Habari

Mashabiki Nchini Kenya Wampendekeza Urban Settlah kuingia Groove Award Kama Mwimbaji Chipukizi.

Na Erick Mutinda-Kenya

Jambo la kushtua wengi kwa kipindi kifupi mwimbaji wa muziki wa injili Kenya Urban Settlah  ametokea kupendwa na kukubalika na mashabiki nchini humu baada ya kuachia wimbo wake wa Nitume ambao unafanya vizuri kwenye media mbalimbali hapa nchini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mashabaki hao wamesema kwamba uimbaji wa Settlah ni wa tofauti na ambao unamfanya mtu aweze kukaa karibu na Mungu kutokana na utaalamu wa tungo zake ndicho kilicho wafanya kuomba waandaaji wa tuzo za Groove waweze kumkumba katika kipengele cha mwimbaji Chipukizi wa Mwaka’

‘Urban Settlah anatubariki sana japo si mwimbaji wa muda mrefu sana lakini tumempenda na tuna muelewa hivyo tunaomba waandaaji wa tuzo hizi za Groove waweze kumuweka katika nafasi ya mwimbaji anayechipukia huu wimbo wake wa Nitume unafanya vyema sana”Alisema mmoja wa mashabiki wa Urban.

kwa upande wake Urban Settlah alieleza kuwa anawashukuru mashabiki zake hao kwa kumpendekeza katika tuzo hizo anawashukuru sana.”Kwa binafsi nawashukuru sana wote ambao wanasapoti kazi zangu tangu ile ya Kimbilio na albamu yangu ya pili ya Rejesha pamoja na hii video yangu mpya ya Nitume ambayo ndiowanaiomba iingie kwenye tuzo kama video bora ya mwimbaji anayechipukia so niwaambie kuwa tuombe Mungu likifanikiwa ombi lao basi fanya yale wanatakiwa kufanya’‘Alisema Urban Settlah

Mbali na uimbaji Urban kwa taaluma na Mwandishi wa habari na mpaka sasa ana Albamu zake mbili ya Kimbilio na Rejesha pamoja na Video ya Nitume ambayo inafanya vyema hapa nyumbani, ameshiriki matamasha mbalimbali kama Groove tour, Mwafaka Award, Golden platform concert na mengine mengi.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Rogate Kalengo wa GSS(2016)Dar Kufanya Uzinduzi wa Albamu yake April 23 Mwaka Huu.

Next post

Sikiliza & Download GospelMusic Audio: Ritha Komba - Kivulini