Connect with us

Mario Lopez abatizwa, katika mto aliobatizwa Yesu

Habari

Mario Lopez abatizwa, katika mto aliobatizwa Yesu

Na mwandishi wetu,

Muigizaji na mtangazaji maarufu wa televisheni Mario Lopez amebatizwa katika Mto Yordani huko Yerusalemu Alhamisi ya wiki hii.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 44 aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter kwa kile kilichokuwa kinaendelea katika tukio hilo.

“Tuko kwenye Mto Yordani ambapo Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu Kristo. Mimi pia nabatizwa,” Lopez alisema. “Ni siku nzuri sana. Kuna kuhani wa Kikatoliki ambaye atanifanya kuwa heshima na kuna mahubiri yanayoendelea hivi sasa. Hivyo nitaungana na watu hawa wema kabisa katika ibada hii, aliendelea.

Katika video ya pili, Lopez anaonekana amesimama katika mto Yordani huku waimbaji wakiimba wimbo wa injili “Nimeamua Kumfuata Yesu.”

Huku akiwa ameshikwa na makuhani wawili wa kikatoliki na kumuuliza Mario ikiwa anaamini katika Yesu Kristo na “anataka kumtumikia katika maisha yake yote?” “Ndiyo,” Lopez alisema.

Lopez ameendelea na ziara yake huko mji wa Yerusalemu kwa kutembelea kanisa la Mtakatifu Sepulchre na Via Dolorosa, au kwa kiingereza linavyoitwa  “The Way of the Cross.” (Njia ya Msalaba.)

 

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Habari

To Top