Connect with us

Marekani: Kanisa Lajaza Mafuta Magari 250 Bure na Watu 8 Wakampokea Kristo

Kanisa Lajaza Gesi Magari 250 Bure na Watu 8 Wakampokea Kristo

Top Stories

Marekani: Kanisa Lajaza Mafuta Magari 250 Bure na Watu 8 Wakampokea Kristo

Jumamosi iliyopita, waumini wa kanisa la Greater Mount Calvary Holy Church (GMCHC) lililopo Washington D.C. walijaza mafuta kwenye magari ya watu 250 bure na kufanikiwa kuwaongoza watu nane kwa Yesu Kristo.

Tukio hilo, lililopewa jina la “Gas on God,” lililofanyika katika kituo cha gesi cha BP ambapo washirika kutoka Kanisa hilo waliihudumia jamii kwa kulipia dola 20 za mafuta kwenye magari ya watu 250.

“Bado tunashangaa jinsi Bwana alivyotembea nasi katika tukio letu la “Gas on God,” kanisa lilisema kwenye chapisho lake Facebook. “Ilikuwa baraka iliyoje kuhudumia watu 250 katika jamii yetu kwa kuweka na kulipia gesi yao! Zaidi ya watu 8 walimkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wao! Ilikuwa siku kuu kwelikweli!”

Kristal Woodhouse, Mchungaji Mkuu kanisa hilo la Calvary, alieleza katika video kwamba tukio hilo maalum lilikuwa ni sehemu ya upanuzi wa huduma za kanisa nje ya Kanisa.

“Hii ni nyongeza ya kile tunachofanya kila wiki kama Giving Tuesday – chakula, sabuni za kufulia, pampers n.k,” alielezea. “Lakini mafuta kwenye gari ni jambo la lazima vile vile, Lazima ufike kazini, lazima ufike dukani, lazima ufike kanisani , n.k”

Huku baadhi ya washirika wa kanisa hilo wakiweka mafuta kwenye magari ya watu, Mshirika mmoja aliyejulikana kama Tamar Shaw alichukua hatua zaidi na kuuliza ikiwa kuna mtu anayehitaji maombi. Kwa upande wake, alishuhudia watu wanne wakimkubali Kristo kama Bwana na Mwokozi wao. Kufikia mwisho wa tukio hilo, jumla ya watu wanane waliamua kutoa maisha yao kwa Kristo. “Mafuta ya Bure yamewafikisha hapa. Lakini hii bado ni huduma,” Shaw alidai.

“Tunataka kuwa na nia ya dhati katika kutumikia jamii na kugusa maisha ya watu wengi kwa njia nyingi tofauti,” Dk. Susie C. Owens, mchungaji mwenza wa GMCHC, alielezea. “Yesu alituagiza tuwajali jirani zetu na kuwapenda. Hii ni ishara ya hilo, na tunatumaini kwa namna fulani tumebadilisha maisha yao.”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top