Connect with us

Mambo 7 Muhimu Unayotakiwa Kuyaombea Kila Siku

Mambo 7 Muhimu Unayotakiwa Kuombea Kila Siku

Somo

Mambo 7 Muhimu Unayotakiwa Kuyaombea Kila Siku

Sote tunajua umuhimu wa maombi katika maisha yetu ya kila siku, Wakati mwingine unaweza kuingia kwenye maombi ukakosa cha kuombea na ukabaki kujiuliza nini cha kuombea, Wakati mwingine mahitaji binafsi yanaweza kuamua na kukulazimisha namna utakavyoomba japo si kwa wakati wote.

Leo nataka nikushirikishe mambo saba ya kuombea kila siku, Haijalishi nini kinaendelea katika maisha yako haya ni mambo ambayo unapaswa kuyaombea kila siku kwa sababu yana umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku.

1. Ombea ulinzi wa Watakatifu.
Kuna nchi ulimwenguni ambazo ni ngumu kujitambulisha kuwa wewe ni Mkristo na ukaishi kwa amani. Tunahitaji kuwakumbuka ndugu na jamaa zetu katika Kristo walio katika nchi hizo na kuwaombea. Yohana 17:9-11

2. Ombea Mwili wa Kristo uwe mmoja.
Ikiwa kuna jambo mwili wa Kristo unahitaji ni umoja. Kwa sehemu kubwa duniani Wakristo wamegawanyika sana na hili ni tatizo kubwa. Yesu anatuambia kwa nini hili ni tatizo, kwa sababu kanisa linapogawanyika linaweza kuwazuia watu kumwamini na kumwelewa Yesu ni nani ndio maana unapaswa kuomba Mungu ili abomoe kuta zote zinazogawanya na kulemaza umoja katika kazi ya injili ili kuruhusu wale ambao ni wafuasi wa kweli wa Yesu kuwa kitu kimoja hii si kwa ajili sababu zetu binafsi bali ni kwa ajili ya Injili. Yohana 17:20-21

3. Ombea injili ienezwe ulimwenguni Kote.
Kama waumini wa Kristo, tumeagizwa kwenda na kueneza Injili ya Yesu ulimwenguni hivyo ni vyema uombe ili unapoenda katika maeneo mbalimbali ambayo Mungu atakupeleka akupe nguvu na atengeneze nafasi ndani yako ya kueneza habari njema za injili. Wakolosai 4:3-4

4. Omba Mapenzi ya Mungu yatimizwe.
Jambo la muhimu zaidi la kuombea kila siku ni Mapenzi ya Mungu yatimizwe katika maisha yako. ikiwa kila siku utaomba hili kwa kumaanisha litapunguza mambo mengi niliyotaja hapo awali kwa sababu utajikita katika kile ambacho Mungu anataka tufanye. Mathayo 6:10

5. Ombea Viongozi na mamlaka.
Tunatakiwa kuwaombea viongozi na mamlaka katika ngazi zote, Wakati mwingine tunaweza kuchukulia jambo hili kuwa la kawaida na inaweza kuwa ngumu kwa sababu tunazitazama mamlaka hizi kwa macho ya kisiasa au ya kibinadamu na sio kwa macho ya Kiungu, Hata hivyo, hiyo haitupi sababu ya kutokuwaombea. Tuwe waaminifu kwa kuwaombea na tusiruhusu mitazamo hasi inayoweza kutuzuia kufanya kile Mungu anatamani tufanye. 1 Timotheo 2:1-2

6. Ombea wale wasiomjua Yesu.
Tumezungukwa na watu kila mahali wasiomjua Yesu. Tunakumbushwa katika 1 Wakorintho 3:6 kwamba wengine hupanda mbegu na wengine humwagilia maji lakini Mungu ndiye anayekuza. Tunahitaji kuwaombea wale ambao hawamjui Yesu wasikie injili na kuwaongoza sala ya toba ili wasiukose uzima wa Milele. Mathayo 9:36-38

7. Omba utembee kwenye wito unaostahili.
Jambo la mwisho la kuombea kila siku ni la kutembea katika wito unaostahili ambao Mungu amekupa. Kutembea kwenye wito unaostahili unahitaji ukae katika utiifu, utakatifu, na kumtumaini Mungu mara kwa mara, Unapoishi hivi utaweza kuwa na matokeo bora ambayo Mungu anatamani uwe nayo. Waefeso 4:1-3

1 Comment

1 Comment

  1. Lazaro kalaita

    November 23, 2021 at 10:48 pm

    habari nilikuwa na pakua nyimbo kupitia hata sasa hivi sioni tena je mmetoa huo mfumo kama mmetoa basi naomba urudi asanteni

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top