Habari

Malengo yako ndio mafanikio yako kuzinduliwa 17 March 2018.

Na Mwandishi wetu,
Mwandishi wa vitabu vya hamasa kwa vijana anayefahamika kwa jina la Valeriano Ulrick Mtundu ameweka wazi na kuthibitisha juu ya uzinduzi wa kitabu chake kipya kinachobebwa kwa jina la     MALENGO YAKO NDIO MAFANIKIO YAKO, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa siku ya tarehe 17.03.2017 katika ukumbi wa Landmark Hotel, Ubungo jijini Dar es salaam.

Valeriano Mtundu amesema kuwa tukio hili litakuwa ni la pekee kwasababu ya kusudi lililobebwa ndani ya kitabu hicho ambacho anaamini kitakwenda kuwakomboa na kuwasaidia watu wengi zaidi hasa vijana ambao watamani kupata mafanikio katika mambo mbalimbali ambayo wanafanya na kupata mwanga mpya wa namna ya kuzitumia fursa kupitia malengo yao.

Kwa mujibu wa Valeriano amesema kuwa Tukio hilo litaanza saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni, hivyo amewataka vijana na watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali kujisajili kwa kutuma ujumbe mfupi wa kuthibitisha ushiriki wao katika tukio hilo adhimu kupitia namba zake za simu kama zinavyoonekana hapa chini.

Hakika hii ni fursa kubwa na ya kipekee kwako kijana ambaye unahisi kukata tamaa, kukosa mwelekeo wa nini ufanye ili uweze kupata mafanikio, ni Imani yetu kubwa kuwa kupitia kitabu hiki utapata mwanga mpya wa mpenyo wa mafanikio yako.

Kumbuka hakuna kiingilio, kwa maswali na maelezo zaidi juu ya tukio hili na kitabu hiki waweza kuwasiliana na mwandishi Vareliano Mtundu kupitia Simu namba/WhatsApp: +255 769 006 725
Facebook: Valeriano Mtundu

Karibu sana mwana wa Mungu ni hakika utabarikiwa sana. MALENGO YAKO NDIO MAFANIKIO YAKO.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Judith Mbilinyi - Maisha Yangu

Next post

Video | Audio: SWAG Band - NENO