MAKOSA MATANO WALIYOYAFANYA WAIMBAJI WA GOSPEL MWAKA 2015, BY JOHN PAZIA. - Gospo Media
Connect with us

MAKOSA MATANO WALIYOYAFANYA WAIMBAJI WA GOSPEL MWAKA 2015, BY JOHN PAZIA.

Habari

MAKOSA MATANO WALIYOYAFANYA WAIMBAJI WA GOSPEL MWAKA 2015, BY JOHN PAZIA.

John Pazia, Mtangazaji wa Radio Habari Maalumu na Mdau wa muziki wa Injili amezungumza na GospoMedia.Com na kufunguka kuhusu makosa ambayo ameyaona kwa mwaimbaji wa muziki wa Injili Tanzania kwa mwaka 2015 na miaka mingine iliyopita. baadhi ya makosa hayo ni..
1.UTAYARISHAJI WA KAZI ZAO (VIDEO NA AUDIO)
John Pazia amefunguka kuwa baadhi ya waimbaji hawakutoa kazi nzuri saana na wengine walikurupuka kitu ambacho kinawashusha waimbaji wengi kwenye viwango vyao.
2.KUJITANGAZA(PROMOTION)
“Kama mwimbaji hajitangazi, anatoa kazi anasikiliza yeye na rafiki zake au watu wa kanisani kwake peke yake hawezi kufika mbali”, alifunguka John Pazia. John Pazia aliendelea kwa kusema kuwa waimbaji watumie vizuri vyombo vya habari, isitoshe kwa sasa kuna mitandao ya kijamii, kila Mwimbaji anapaswa kuwa na akaunti facebook, twitter na Instagram.

3.UTUNZI WA NYIMBO
Hapa John Pazia amewachana wale waimbaji ambao toka album ya kwanza mpaka ya mwisho wanaimba vile vile kuanzia melodi mpaka maneno bila kuwa na ubunifu wowote akiweka wazi kuwa hii hutokana na kutosoma neon wala kuwa na maombi.
4.KUTOKUWA NA UMOJA
Kutokana na mahojiano mengi ambayo John Pazia amefanya na waimbaji wengi amegundua kuwa hakuna umoja baina yao hii hupeleka kutoweza kufanya hata kazi za pamoja.
5.WAIMBAJI KUTOKUWA NA USIMAMIZI(MANAGEMENT)
Waimbaji wamekuwa wakifanya vitu vyote wao wenyewe kitu ambacho kimekuwa changamoto kubwa, hauwezi kufanya kila kitu peke yako,butachoka na utakosa muda wa kutengeza nyimbo nzuri na kuomba Mungu, amefunguka John Pazia.
Zaidi John Pazia amewataka waimbaji kuwa na mahusiano mazuri baina ya wao kwa wao na wachungaji pia.

By Sirmbezi
Like our page>>> GospoMedia

More in Habari

To Top