Habari

Makamu wa Rais wa Nigeria Amesema Maendeleo ya Amani ya Nchi, Yapo Kanisani.

Lagos, Nigeria.

Makamu wa Rais nchini Nigeria, Prof. Yemi Osinbajo amewahimiza viongozi wa Kikristo nchini humo wasiyumbishwe na mitazamo mingine ambayo aliita ni mitazamo ya ”ajenda za kiislam” na badala yake wazingatie “ajenda zao za Kikristo”.

Mheshimiwa Osinbajo aliyasema hayo wakati akizungumza na wachungaji huko mjini Lagos katika mkutano unaojulikana kama “Towards a Better Nigeria”, alisema kuwa sehemu ya tatizo katika nchi ya Nigeria kunatokana na kushindwa kwa viongozi wa Kikristo kuchukua nafasi zao na kufanya maamuzi sahihi.

Mh.Yemi Osinbajo, makamu wa Raisi nchini Nigeria.

Kupitia vyombo vya habari vya ndani, Mh.Osinbajo alisema: “Sehemu ya tatizo la nchini yetu kunatokana na kushindwa kwa viongozi wa kikristo kutumia nafasi yake vizuri. Tumeyaelekeza mawazo yetu juu ya kitu tunachokiita ajenda ya Kiislam, Tunakitafuta kila mahali kama tunatafuta mapepo. Lakini ziko wapi ajenda za wakristo. Je, hatuna haki? sisi pia tumegawanywa kama wakristo ili tuwe na ajenda. Jambo la umoja na maendeleo ya nchini yetu ya Nigeria upo ndani ya kanisa, “alisema kwa ujasiri siku ya Jumapili.

Makamu wa rais wa Kikristo aliikosoa Serikali ya Shirikisho juu ya utoaji wa dhamana isiyo ya riba ya Kiislam, inayojulikana kama sukuk. Makamu huyo alisema: “Sukuk ni dhana ya Kiislamu, ambayo inawezesha watu kupata upatikanaji wa mikopo kwa urahisi na kutumika kama dhamana.

Nigeria imekuwa mwanachama wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (Islamic Development Bank) mwaka 2005, ambao kusudi lake ni kukuza maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya kijamii ya nchi wanachama na jumuiya za Waislamu kwa pamoja kwa mujibu wa kanuni za Shariah, (Sheria ya Kiislam).

Kulingana na Kituo cha Utafiti cha Pew, Nchi ya Nigeria ina idadi kubwa zaidi ya wakristo kuliko nchi yoyote Afrika, ambapo watu zaidi ya milioni 85 nchini Nigeria ni waumini wa makanisa ya madhehebu mbalimbali.

Mh.Yemi Osinbajo

Mh.Osinbajo pia alizungumzia kuhusu kushughulikiwa kwa suala la rushwa.
Alisema: “Hakuna taifa juu ya uso wa dunia hii ambalo linaweza kuendelea kuishi chini ya mizigo ya rushwa ambayo nchi yetu ilikuwa inapitia changamoto hiyo. Wasomi wa Nigeria, bila kujali tofauti zao za kisiasa, dini au kabila ambao wote kwa kiasi kikubwa tunasukumwa na nia moja. Wao ni ubinafsi, hawajajiandaa kujitoa sadaka katika huduma ambazo viongozi wa jamii huzifanya. Rushwa ya kiwango cha hali juu haijui dini, ukabila au mambo mengine. Tunapaswa kushughulikia suala la rushwa kwa uwazi. Mfumo wa maisha yetu kama jamii na nchi kwa umetawaliwa na rushwa. Huu ni wakati wa kujenga na Tunaweza kuwa taifa imara la zaidi la Afrika kwa wakati ujao. ”

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Je unazifahamu njia za asili za kukabiliana na kwikwi? Soma hapa ujifunze.

Next post

Music Audio: Godfrey Mnakum - Tangulia Mbele