Connect with us

Audio: Magreth Ndola – Uhimidiwe

Audio

Audio: Magreth Ndola – Uhimidiwe

Kutoka jijini Mwanza mtumishi na mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Magreth Ndola ameachia wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2018 uitwao Uhimidiwe, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Faith Music Lab chini ya mikono ya prodyuza George Kabano.

“Uhimidiwe ni wimbo wa shukrani yangu kwa Mungu kwa yale aliyotenda katika maisha yangu, Ni kweli nilipita katika mambo magumu sana na hii ndio sababu ya kuandika wimbo huu nikiwa na lengo la kuwapa matumaini watu ambao wanapita katika kipindi kigumu, Natamani wimbo huu umguse kila mmoja na kumsisitiza kuwa asife moyo ajue kuwa yupo Mungu anayeweza kumvusha kama mimi nilivyo vuka japo haikuwa rahisi ila ni kwa neema ya Mungu kupitia imani, Amini jana yako sio kesho yako. Waebrania 11:1 Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.” – alisema Magreth Ndola

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri nikiamini kuwa utakukugusa na kukuinua, Barikiwa!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Magreth Ndola kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 763 479 520
Facebook: Magreth Ndola
Instagram: @magrethndola

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top