Habari

Magaidi wa Kiislamu wamshikilia Msichana wa Kikristo Kwa sababu Alikataa Kumkana Kristo

Na Mwandishi wetu,

Msichana Mkristo aitwaye Liya Sharibu ameripotiwa kuwa amefungwa na magaidi wa kiislamu nchini Nigeria kwa sababu alikataa kuikana imani yake ya ukristo.
Siku ya Jumatano, kundi la kigaidi linalojulikana kama Boko Haram lilirejesha wasichana 101 kati ya 110 ambao walikuwa wamechukuliwa kutoka kwenye shule yao kaskazini mashariki mwa nchi ya Nigeria mwezi uliopita.

Mmoja wa wasichana walioachiwa huru na kundi hilo la kigaidi alisema Sharibu hakutolewa kwa sababu alikuwa mkristo.

“Alikuwa amefungwa,” alisema Khadija Grema. “Tulifunguliwa kwa sababu sisi ni wasichana wa kiislam na hawakutaka tuteseke, ndiyo sababu walituachilia.”

Amira Adam Mohammed mwenye umri wa miaka 16, ambaye pia alikuwa miongoni mwa wale walioachiliwa na magaidi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Boko Haram wataendelea kumshikilia Sharibu mpaka atakapobadili dini.

“Kama atabadili dini, watamtoa,” alisema Amira.

Amira na wasichana wengine walitekwa nyara Februari 19 wakati kundi la watu 50 wenye silaha waliishambulia shule huko mjini Dapchi, mji wa jimbo la Yobe nchini Nigeria.

Baba wa Sharibu, Nata Sharibu, alisema baadhi ya wasichana walioachiliwa walimwambia kuwa binti yake alikataa kumkana kristo na ndiyo sababu yeye hakuachiliwa na magaidi.

“Binti yangu yupo hai lakini walisema ni mkristo na ndiyo sababu hawawezi kumtoa,” Sharibu aliiambia redio ya RayPower 100.5 FM nchini Nigeria. 

“Walimpa nafasi ya kubadili msimamo wake ili aweze kutolewa lakini binti yangu alisema hawezi kuwa Muislamu.”

Boko Haram, ni neno ambalo katika lugha ya Kihausa ina maana kuwa “Elimu ya Magharibi ni marufuku” likiwa ni kundi kubwa la Kiislam ambalo lina itikadi kali.

Sharibu alisema alikuwa na furaha kwa wazazi wengine ambao binti zao walikuwa huru, na akaongeza: “Mimi pia ninafurahi pia kwa sababu binti yangu hakumkana Kristo.”

Kundi la haki za kibinadamu la Nigeria limemwomba rais wa nchi kuhakikisha Sharibu anarudi salama.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Emy Dimking – Nobody Like You

Next post

Video | Audio : Eben - Joyful Noise