Habari

Madam Flora Atema Cheche Kwa Wanaomchafulia Jina lake Mitandaoni

Mwimbaji Mkongwe wa muziki wa Injili Tanzania Madam Flora awali alifahamika kama Flora Mbasha amewaonya wale ambao wanamchafulia jina lake wakizani kwamba hawafahamu amesema sheria itachukua mkondo wake kama wataendelea na tabia yao ya kumchafulia jina lake.

Ameandika katika Group lake la Whatsapp liitwalo ‘‘Wakati Wake Video”akikanusha habari ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii akidhaniwa kuwa amefanya mahojiano na moja ya kituo na kusema maneno ambayo yeye binafsi amesema hakuyasema na wala hajafanya mahojiano na kituo chochote licha ya kuachia kitabu chake cha Siri za Flora Mbasha.

‘Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na radio yoyote na kuzungumza maneno hayo kama ilivyo sambaa mitandaoni. Naomba mzipuuze maana ni mpuuzi mmoja tu ameamua kuonyesha upuuzi wake na kutafuta Followers kwenye page yake. Na niseme tu kwamba hivi sasa sitakaa kimya tena, Huyo aliyezoea  kunizushia story za uongo akifikiri siijui sheria ajipange vizuri maana mahakama ipo na sheria ipo, narudia tena kusema habari hii iliyosambaa mitandaoni ni ya uongo sijazungumza mimi maneno hayo@flora_madam Kitabu ndio kimetoka last wiki cha ‘SIRI ZA FLORA MBASHA’lakini sijafanya interview yoyote na kuongea upuuzi huo kama ilivyosambaa”Aliandika Madam Flora.

Madam Flora kwasasa anatamba na wimbo wake wa Wakati Wake ambao upo ndani ya Albamu yake mpya ambayo ataiachia hivi karibuni pia Madam Flora anakitabu chake ambacho amekiandika na kukipa jina la SIRI ZA FLORA MBASHA.

Kwa mawasiliano na Madam Flora:

Simu/WhatsApp +255 758 105 014
Facebook: Madamm Flora Henry
Instagram: @flora_madam
YouTube: Madam Flora

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Download Audio: Agent Snypa - Unconditional

Next post

Moses Simkoko, Sifaeli Mwabuka Wapishana Kauli Juu ya Kusheherekea Siku ya Kuzaliwa.