Connect with us

Audio: Machalii Wa Yesu – Ndoa

Muziki

Audio: Machalii Wa Yesu – Ndoa

Kutoka jijini Arusha leo nimekusogezea wimbo mzuri uitwao Ndoa kutoka kwa kundi mahiri la muziki wa Injili kwa mtindo wa Hip Hop linalofahamika kwa jina la Machalii wa Yesu, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Cuckaz Beats chini ya mikono ya prodyuza Justinoo.

“Wimbo huu umeandaliwa kama zawadi maalum kwa mmoja wa kundi la Machalii wa Yesu anayefahamaika kwa jina la T More siku ya harusi yake iliyofanyika Aprili 7, 2018. Na sasa wimbo huu umeachiwa rasmi kwa wanandoa wote na kuwahamasisha wale ambao wapo njiani kuelekea kwenye maisha ya ndoa.

Ndoa, ni wimbo maalum kwa maharusi, wanandoa na wapendanao wote walio katika safari ielekeayo kufunga agano la kuwa pamoja katika maisha yao. Pia ni inspiration kwa vijana wote mwisho wa siku wafanye maamuzi haya ya kumbariki Mungu na staha kwa jamii.” – Walisema Machalii wa Yesu

“Anayempata mke amepata bahati njema; hiyo ni fadhili kutoka kwa Mwenyezi-Mungu.” – Methali 18:22, Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina amini kuwa utakubariki na kukuhamasisha wewe ambaye unatarajia kuingia kwenye maisha ya Ndoa, Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na kundi la Machalii wa Yesu kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 719 915 008
Facebook: Machalii wa Yesu
Instagram: @machaliiwayesu
Twittter: @machaliiwayesu
Youtube: Machalii Wa Yesu

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TRENDING

To Top