Habari

MAASKOFU WA AUSTRALIA MATATANI KWA KUSAMBAZA KIJARIDA CHA NDOA YA “MKE NA MUME”

Maaskofu nchini Australia wamejikuta kwenye mgongano na wanachama wa wa kile kinachoitwa “gay marriage political Movement” ambao wanatetea maslahi ya watu wenye ndoa za jinsia moja (ndoa za kishoga) baada ya kusambaza kijarida chenye ujumbe unaohusu ndoa ya halali kwa wakristo yani ile ya Mume na Mke. Kijarida hicho chenye jina la “Don’t mess with marriage” kilisambazwa nchi nzima na pia inadaiwa askofu Julian Porteous wa Hobart alituma kijarida hicho kwenye shule za watoto wa kikatoliki huko Tasmania. Hatua hiyo imemkasirisha Bw.Rodney Croome,kiongozi wa mapambano hayo ya kutetea watu wenye ndoa za jinsi moja na kudai kuwa maaskofu hao wanawatumia vibaya watoto kwa kuwapa mtazamo unaokandamiza ndoa za jinsia moja kwa kuwapa kijarida hicho. Mwanasiasa kutoka Left Wing Austrilian Party, Bw.Martine Delany amefungua kesi ya malalamiko kuhusu tukio hilo huku Baraza la maaskofu la katoliki nchini humo wamepewa siku 21 kujibu tuhuma hizo kabla kesi haijafika mahakama kuu.

As reported by: Carrie Dedrick

Advertisements
Previous post

VIDEO: MALUDA FEAT JULIANI - EASY

Next post

UHURU WA KUABUDU KWA WAKRISTO INDIA NI KITENDAWILI