Uncategorized

MAARIFA: MAKOSA UNAYOWEZA FANYA KAMA UNA USHAWISHI MKUBWA

Tunajua uongozi ni ushawishi. Ushawishi unaweza kuwajenga watu au kuwabomoa watu kulingana tu na ufahamu wa mwenye ushawishi. Wengi tumejikuta tunaharibu watu bila kujua Sababu ya nguvu ya ushawishi tuliyonayo. Ni ukweli kuna baadhi ya watu wachache huwa na ushawishi kwa watu wengi. Anapofanya au kuongea kitu kinaathiri wengi katika hali chanya au hasi. Pamoja na kuwa wenye ushawishi ni wachache ila wanaoutumia ushawishi vizuri ni wachache zaidi. Tunapozungumzia ushawishi hatuwezi acha zungumzia uongozi. Sababu kama unaoushawishi basi wewe ni kiongozi. Kama upo katika kundi la watu basi unaweza kuwa kiongozi nyuma ya Pazia au mbele ya pazia ( Nafasi).pp4

Kosa la kwanza ni kutokujua unachofanya na kuongea kinasikilizwa na kupokelewa na watu kwa namna tofauti na wengine wakifanya au kuongea. Unapokuwa unaushawishi neno dogo utakalosema litachukuliwa kama mfano huko mbele hata Kama ulilisema kwa utani au kawaida bila kulitilia mkazo. Nimeharibu wengi hapo sababu naweza nikaongea kitu kwa utani au kawaida cha ajabu nakuja sikia Makwaya alisemaga hiki ni lazima kiwe hivi. Unapokuwa na ushawishi kuwa makini na maneno na matendo maana wengi wamekosea na kupoteza wengi hapo.

Kosa la pili ni ile hali ya kuchukulia wote wanaufahamu kama wa kwako. Au wanaona vitu kwa namna unavyoona. Tunasahau kwamba kuwa na ushawishi wa hali ya juu ulionao imekuchukua miaka mingi ya kukosea na kupatia. Miaka mingi ya kuanguka na kusimama. Semina nyingi, Vitabu vingi, kuongozwa na watu wengi, kuishi kwingi nk. Hivyo leo unapochukulia watu wote wanaufahamu sawa na wewe hivyo unaongea na kufanya chochote mbele yao. Badala ya kuwatengeneza unakuwa unawaharibu. Sababu watataka kuwa kama wewe na hawajui kuwa imekuchukua miaka na shuruba nyingi kuwa hivyo ingawa wao watataka kwa mwaka mmoja wawe Kama wewe .Gospomedia

Kosa lingine ni kutamani kusikilizwa kila unachosema. Sikatai ni kweli unaushawishi mkubwa lakini huo ushawishi usikupelekee kutaka kusikilizwa kila kitu. Kuna uhitaji wa kuwa makini katika hili. Kuna mambo wala huitajiki kushauri au kuingilia ni ya kukaa pembeni. Lakini kuna mambo ya kushauri na sio lazima ushauri wako ufuatwe kama ulivyoshauri. Unaweza fuatwa tofauti kidogo na ulivyoshauri au usifuatwe kabisa na mambo yakaenda vizuri.

Lakini pia kosa lingine ni kutokuwa mwepesi wa kuomba msamaha. Watu wengi wakishakuwa na nguvu kubwa ya ushawishi husahau kabisa neno nisamehe. Ushawishi kwa upande mwengine ni ubabe usiotumia mabavu kumfanya mtu afanye jambo. Sasa tafakari jinsi ilivyo kazi kwa wababe wengi kuomba msamaha hata kama wamekosea. Ushawishi wako haukufanyi kwamba huwezi kukosea. Na pale unapokosea huna budi kuomba radhi. Sababu usipofanya hivyo unapoteza ushawishi ulionao taratibu.Gospomedia

Kosa kubwa la mwisho. Ni kutengeneza maadui bila kujua. Unavyozidi kuwa na ushawishi alafu ukawa unafanya makosa tuliyoongelea hapo juu kinachofuata unakuwa unatengeneza maadui wengi wa chinichini. Na kama u kiongozi basi ujue uongozi wako hautakuwa na nguvu tena. Sababu utakuwa na watu wengi wanakusikiliza kwa masikio wakati mioyo yao haisikilizi kabisa na jamii Inakuchukia mbaya wakati inawezekana hapo mwanzo ni wewe ndiye uliyewashawishi kufanya mambo mengi mazuri wanayoyafanya.

Kama ambavyo huwa tunajitengeneza ndivyo huwa tunajiharibu kwa kutokuwa makini sababu tu tunaushawishi.

Imeletwa kwenu na Mwl. Emmanuel Makwaya
©TO BE IS TO DO

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
goodluck gozbert
Previous post

NYIMBO ZA GOODLUCK GOZBERT SASA KUPATIKANA iTunes.

Next post

VIDEO KUMI BORA ZILIZOFANYA VIZURI MWEZI WA NNE 2016. HIZI HAPA