Connect with us

Maajabu ya MUNGU: Je wajua kazi ya sharubu za paka?

Maarifa

Maajabu ya MUNGU: Je wajua kazi ya sharubu za paka?

Mara nyingi paka wa nyumbani huwinda usiku na imegundulika kwamba sharubu huwasaidia sana kutambua vitu na kuvikamata wakiwa katika mawindo hasa baada ya giza kuingia.

Sharubu za paka zimeunganishwa na tishu zenye neva nyingi za fahamu. Neva hizo zina uwezo mkubwa wa kutambua hata msukumo mdogo wa hewa. Hivyo, paka wana uwezo wa kutambua vitu vilivyo karibu nao bila kuviona, jambo linalowasaidia sana kunapokuwa na giza, Kwasababu sharubu zina uwezo wa kutambua shinikizo la hewa, paka huzitumia kujua mahali na mwendo kitu fulani. Pia, sharubu humsaidia paka kupima upana wa sehemu fulani kabla ya hajaingia. Kitabu kiitwacho Encyclopædia Britannica, kinasema kwamba “kazi ya sharubu (vibrissae) inajulikana kwa kiwango kidogo tu; hata hivyo, paka hulemaa kwa kipindi fulani kama sharubu hizo zikinyolewa.”

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wanasayansi wanabuni roboti zitakazokuwa na vipokezi vinavyofanya kazi sawa na sharubu za paka ili kusaidia roboti hizo kutembea katika maeneo yenye vitu vingi bila kukwazwa.

Ali Javey, mwanasayansi katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley amesema kwamba vipokezi hivyo vinavyoitwa e-whiskers: Vitatumia programu mbalimbali za kompyuta kwa ajili ya roboti za kisasa, zilizo rahisi kutumiwa na watu na zitakuwa pia na programu za kibiolojia.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Maarifa

To Top