Connect with us

Music Audio: Liza J – Nakupenda Pia

Muziki

Music Audio: Liza J – Nakupenda Pia

Kutoka jijini Dar es salaam Tanzania, leo nautambulisha kwako wimbo mzuri uitwao Nakupenda Pia kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Liza J. wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Faith Music Lab chini ya mikono ya producer George Kabano.

Nakupenda Pia ni wimbo wa sifa na shukrani unaoelezea upendo mkuu wa Mungu ambao hauna mipaka katika maisha yetu kupitia Yesu Kristo ambaye aliamua kuja duniani ili kutuweka huru na kujenga uhusiano wetu mpya na Mungu na upendo wake kwetu ukaenda mbali zaidi kwa kukubali kuteseka na kufa msalabani ili mimi na wewe tuweze kupata ondoleo la dhambi, hakika upendo huu ni wa pekee sana kwetu kwa maana hakuna mahali ambapo unapatikana zaidi ya kwake pekee hadi leo Yesu bado anatupenda licha ya binadamu kujisahau na kuendelea kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu lakini bado Yesu anatupatia nafasi ya kurudi kwake, kuomba msamaha na kutuweka huru na hapo ndipo unashukuru na kukiri kwa kusema Yesu Nakupenda.

Ni moja kati ya nyimbo nzuri ambazo nina hakika utabarikiwa nayo kila wakati utakapokuwa unaisikiliza. Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu. Mungu akubariki sana!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Liza J. kupitia
Simu/WhatsApp: +255 621 873 145
Facebook: Liza J.
Instagram: @lizaudawa
Twitter: @lizaj
YouTube: Liza J.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top