Audio

Audio: Lester – Step On The Pedal

Mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Lester kutoka nchini Zambia ameachia wimbo wake mpya uitwao “Step On The Pedal” muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Ino.

“Step On The Pedal” ni wimbo unaoungumzia bidii katika kumtafuta Kristo ni wimbo unaowasisitiza wakristo kuendelea kusonga mbele katika kutafuta wokovu wao na wokovu wa watu wengine, Wimbo huu unatukumbusha kwamba kushinda kifo na kutupa tumaini la wokovu kwa Bwana wetu Yesu kristo, ni mwanzo tu wa safari yetu katika jitihada za kupata uzima wa milele. Sehemu iliyobaki ipo upande wetu kwa sababu safari yetu kuelekea katika wokovu kamili sio kazi rahisi, imejaa vikwazo ambavyo vinaweza kuturudisha nyuma ikiwa hatuwezi kuvumilia! MUNGU awe pamoja nasi kupitia mwanaye wa pekee, YESU KRISTO!

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri ambao nina hakika hautaacha kusikiliza kila wakati ikiwa ni moja kati ya kazi nzuri ambazo mbali na ujumbe ulio katika wimbo huu bali hata uimbaji na mpangilio wa muziki huu utakufanya uufurahie upendo wa Mungu katika maisha yako, Ameen.

 

Download Audio

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Chengelo - Agape Love

Next post

Audio: Protek illasheva Feat. Frank Edwards & Nsikak – Ngalaba