Connect with us

Music Audio: Lenjima Feat Stewart – Usinipite

Muziki

Music Audio: Lenjima Feat Stewart – Usinipite

Kutoka mjini Moshi, leo kwa mara nyingine tena nakukaribisha kusikiliza wimbo mzuri uitwao Usinipite kutoka kwa rapa mpya wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Lenjima hapa akiwa amemshirikisha Stewart, Wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Range93 chini ya mikono ya prodyuza Capacity.

Baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza uitwao Impossible na kufanikiwa vyema na kuingia kwenye chati za kumi bora mwezi wa saba zinazoachiwa na tovuti ya gospomedi.com, leo tena rapa huyu ameachia wimbo huu uitwao Usinipite ukiwa ni wimbo uliobeba ujumbe wa matumaini kwa watu ambao wanapita kwenye changamoto mbalimbali za kimaisha na kupitia wimbo huu Lenjima anasisitiza watu wote ambao wanahisi kukata tamaa warudi kweye maombi na kumsihi Bwana Yesu awakumbuke kwa hayo ambayo wanapitia na kwa uwezo mkuu wa Mungu wataweza kuokolewa na kufutiwa matatizo yao.

”Wimbo huu ni wa kumuomba Mungu kumsihi asitupite katika maisha yetu ya kila siku, pia nimegusa makundi kadhaa ya jamii kama vile Yatima, Wajane, Wanafunzi na ajira kwa vijana yakiwa ni makundi ambayo yanakutana na changamoto kubwa katika jamii yetu ya leo naamini Mungu atawasikia na atafanya jambo la kurudisha tumaini lao.” – Lenjima

Rapa Lenjima kwasasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha ushirika Moshi MoCu ambaye mbali na kuimba muziki wa Injili bado pia ni mwandishi mzuri wa nyimbo Injili.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye ujumbe mzito kwa jamii ya wana wa Mungu naamini utaungana na rapa Lenjima katika kuwatia tumaini watu ambao wanapitia majaribu na magumu. Mungu akubariki.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na rapa Lenjima kupitia:
Simu: +255 679 381 299
Facebook: Erick Lenjima
Instagram: @erick_lenjima

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top