Habari

Kutoka Nigeria: Download Wimbo Mpya kutoka Muimbaji Jahdiel – Everything is Well.

Muimbaji maarufu kutoka nchini nigeria anayefahamika kwa jina la Jahdiel ameachia single yake mpya, iitwayo Everything is well (“Kila kitu ni kizuri”) wimbo huu ni wa sifa ukiwa umebeba baraka za Mungu na wenye kukuinua sana moyo kila utakapousikiliza.

Akiongea na vyombo mbalimbali vya habari muimbaji Jahdie amesema wimbo huu umeimbwa kwenye mtindo na mahadhi ya muziki wa kisasa tofauti na ile iliyozoeleka na wengi katika tasnia ya muziki wa Injili, hivyo ametumia mtindo huo ili kufanya muziki wake usikilizwe na watu wote na iwe rahisi kuimbwa na kila mtu wa kila rika na hapo amefaulu kusambaza Injili kupitia mashairi yaliyobeba utukufu wa Mungu kwa watu wake kwa kiasi kikubwa.

Hivi karibuni Jahdiel amekuwa katika ziara mbalimbali za muziki nchini Uingereza, Marekani, Afrika Kusini na Zimbabwe mara baada ya kuachia wimbo wake uitwao “Just Like You” ambao aliuachia miezi michache iliyopita na bado anaendelea kuachia nyimbo mpya ambazo hakika zimekuwa baraka kwa watu wengi zaidi duniani.

gospomedia.com inakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu “Everything is Well” na uwe baraka kwako na kwa watu wote. Karibu!!

Download Audio
Facebook page: Jahdiel Benjamin
Instagram: @jahdielofficial
Twitter: @jahdielofficial
YouTube: Jahdiel Benjamin

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Download Music Audio: Gifted - Ni Mungu

Next post

Kutoka Nigeria: Download Wimbo Mpya Kutoka Kwa Ur Flames - I dont Want This To End