Maarifa

Kutana na Mueritrea Haben Girma, kiziwi na kipofu wa kwanza kuhitimu chuo kikuu cha Avard Marekani

Unapotaka kulalamika fikiria tena kwanini huwezi kufanya jambo Fulani ama kufanikisha jambo lolote, mfikirie msichana huyu  Haben Girma ili upate nguvu ya kusonga mbele.
Haben Girma ndiye mwanafunzi mwenye ulemavu wa kiziwi na kipofu ambaye amekuwa wa kwanza kuhitimu shule ya sheria katika chuo cha Avard nchini Marekani. Kwa sasa, mwanamke huyu Mueritrea Haben Girma mzaliwa wa Marekani anapigania nafasi nzuri na elimu bora kwa viziwi na vipofu wenzake duniani kote.
Katika maelezo yake katika Ikulu ya Marekani (White House), Haben Girma alielezea habari ya kaka yake huko Eritrea, Bibi yake Haben Girma alipompeleka kaka yake  Girma shule, aliambiwa viziwi na vipofu hawawezi kufundishwa. Ni jambo lisilowezekana.
Katika umri wa miaka 16, katikati ya vita vya Eritrea vilivyodumu kwa miaka 30, wakipigania uhuru kutoka kwa waethiopia, Mama yake Girma alitembea kwa wiki tatu, akipita katikati ya jangwa la mpaka alipofika kambi za wakimbizi wakamsaidia na kumpeleka kuishi marekani.
Haben Girma alizaliwa Marekani na alikuwa kama Mama yake kiziwi na kipofu, naye pia alikuwa kiziwi na kipofu.
Lakini Marekani ilikuwa tofauti kimtazamo juu ya elimu kwa walemavu. Unavyoweza kupata picha kwamba hiyo ilikuwa tofauti sana na nchini kwake.
Haben sasa ana umri wa miaka 27, hutumia elimu yake ili kusaidia wengine
“Kuhitimu Harvard shule ya sheria inaelezea vizuri nini chaweza kufanyika ukiwa na nia nzuri”
Aliweza kufanikiwa kwa kutumia kifaa kiitwacho “Braille” ambacho hutumiwa na vipofu, kuandika kwa alama zinazoweza kuguswa na kuhisiwa kwa vidole na baobonye (keyboard) kwaajili ya mawasiliano.
HABEN GIRMA3

Haben Girma akiwa ikulu ya marekani akiongea na Raisi Barack Obama kwa njia ya kifaa maalumu kinachoitwa “Braille”

Alipokwenda ikulu mwanzoni mwa mwaka huu, alipokuwa akutana na walemavu wengine pia, raisi Obama alitumia teknolojia kuwasiliana naye.
Haben Girma akasema “Tuma ujumbe kwa jamii yote ya Marekani na ulimwenguni mwote kwamba, watu wenye ulemavu wanaweza tumia vipaji vyao katika jamii zao, wasidharauliwe”
Hivi sasa ni mwanasheria na anashughulika na haki za walemavu California, kuhakikisha kwamba wanafunzi wengine hawakutani na changamoto za kutumia teknolojia kama yeye na kaka yake walizokutana nazo.
Haben Girma akiwa ameshika cheti cha kuhitimu chuo kikuu cha harvad marekani.

Haben Girma akiwa ameshika cheti cha kuhitimu chuo kikuu cha Avard marekani.

Hili ni fundisho kwamba unapotafuta sababu ya kutofanya jambo mfikirie Girma, mlemavu mwanasheria, asiyeona wala kusikia. Kila mtu ana uwezo wa kufanya mambo makubwa sana, usikate tama amua leo na ulete mabadiliko siyo kwako tu bali katika familia, kanisa, jamii, nchi yako na ulimwengu mzima, kuna watu wengi sana wanahitaji msaada wako, amka toka katika mapumziko yanayokulemaza, Mungu hakukuumba ili uwepo tu duniani bali kuna kusudi maalum sana.
Advertisements
Previous post

Download wimbo mpya wa mwana kutoka ONEHOPE PROJECT

Next post

VIDEO: SHEKINAH-JACKIE KOTIRA