Gospo Media ni kampuni(taasisi) inayojihusisha na utoaji wa huduma ya habari na matangazo ya kazi zinazoihusu Injili na jamii, nchini Tanzania.

Gospo Media inamiliki tovuti iitwayo gospomedia.com ikiwa ni chanzo kikubwa cha habari za kikristo kwa kiswahili mtandaoni. Gospo Media pia inamiliki stesheni moja ya redio mtandaoni iitwayo Gospo Radio, stesheni moja ya televisheni mtandaoni iitwayo Gospo TV na gazeti moja la kikristo linalopatikana mtandaoni liitwalo Quality Magazine.

Neno ”GOSPO” ni kifupi cha maneno matatu yaliyo katika lugha ya kiingereza ”Gospel, Spreading, Power” yakimaainisha ”Nguvu ya kueneza Injili” kupitia chombo hiki cha habari(media).

MAONO
Kuwa chombo bora kinachotoa huduma ya habari za kikristo na matangazo yanayohusu kazi
za Injili na watenda kazi wake.

LENGO KUU
Kuihudumia jamii kwa ufanisi katika utoaji wa huduma bora ya habari za kikristo na jamii, pia
kuzisaidia taasisi, makanisa na watumishi mbalimbali katika kuitangaza Injili ya Yesu Kristo ili kuweza kuifikia
jamii yenye uhitaji wa neno la Mungu, huduma za kiroho na jamii.

HISTORIA

Gospo Media imeanzishwa rasmi na kupata kibali cha kisheria mwaka 2016 chini ya usimamizi wa vijana wawili ambao ni Ladslaus Milanzi na Aloyce Mbezi ambao kwa pamoja waliungana katika kufanya kazi ya Mungu kupitia chombo hiki cha habari ambacho kinatumika kutangaza kazi za Injili kama vile habari za kikristo, nyimbo za muziki wa Injili, mahubiri, mafundisho ya kikristo, Mikutano, Matamasha na makongamano ya Injili.

Makao makuu ya Gospo Media yako jijini Dar es salaam, nchini Tanzania.