BurudaniHabari

Kongamano Kubwa la Wanawake Waombolezao Kufanyika Julai 20, 2017. Usipange Kukosa Hii.

Lile kongamano kubwa la wanawake waombolezao kitaifa kwa mara nyingine tena litafanyika Julai 20 hadi 22 mwaka huu wa 2017.

Akiongea na mwanahabari wa gospomedia.com Pastor Debora Malassy ambaye ndiye mratibu wa kongamano hili amesema kuwa kongamano hili ni la aina yake kwakuwa linajumuisha wanawake wawakilishi kutoka mikoa yote ya Tanzania ikiwamo Zanzibar na Pemba. Pia kutakuwa na wanawake kutoka nchini mbalimbali kama Kenya, Zimbabwe, Africa kusini na Marekani.

Kongamano hili limeandaliwa na makanisa na huduma mbalimbali na kuratibiwa na TANZANIA Fellowship of Churches na litafanyika katika ukumbi wa Mtana, Millennium Tower ghorofa ya kwanza kuanzia saa saba mchana.

Makamu wa Raisi – Mh. Samia Suluhu

Mgeni rasmi kwenye kongamano hili la wanawake waombolezao kitaifa anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Samia Suluhu. Shiriki kuomba na kuwa shahidi wa matendo makuu ya Mungu juu ya Taifa la Tanzania. Hakika usipange kukosa na wote mnakaribishwa.

Kwa mawasiliano piga simu juu ya kongamano hili na jinsi ya kufika tafadhali wasiliana na wahusika kupitia

Simu/WhatsApp: +255 754 515215 au +255 769 493 252.

 

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mkesha Wa Shukrani Ya Kumaliza Nusu Mwaka Kufanyika Jijini Dodoma

Next post

Hizi Ndizo Nyimbo Kumi Bora Zilizofanya vizuri Mwezi wa Tano 2017.