Connect with us

Video | Audio: Kome Udu – Show Me Your Glory

Audio

Video | Audio: Kome Udu – Show Me Your Glory

Kome ni mwimbaji wa nyimbo za Injili mwenye asili ya la taifa Nigeria akifanya huduma ya uimbaji nchini Uingereza, Na sasa ameachia wimbo wake mzuri wa kuabudu uitwao “Show Me Your Glory”, Video hii imeongozwa na director IYKE ECHE kutoka studio za HS Ideas media, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za AGM Records chini ya mikono ya prodyuza Evans Ogboi.

“Show me Your Glory ni wimbo ambao ulikuwa ndani yangu toka kipindi ambacho nilikuwa namtafuta sana Mungu aweze kujifunua katika maisha yangu kama alivyoniita katika kazi yake.  “Show me Your Glory” ni maombi ya muda mrefu ambayo yamedhihirisha majibu yake. Ni maombi yangu sasa kwa kila mtu anayetafuta Utukufu wa Mungu, kwamba asichoke kuomba na kuamini kwakuwa utukufu wa Mungu ni wa kweli. ” – alisema Kome

Kome ni moja kati ya waimbaji wachache wenye kipaji kikubwa cha uimbaji na uandishi wa nyimbo za Ibada kwa zaidi ya takribani miaka 25 iliyopita, Wimbo huu upo kwenye albamu yake ya nne inayobebwa kwa jina la “Spirit Overflow” ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo kumi ikiwa tayari imeshaachiwa tangu Juni 30, 2018.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii, Nikiamini kuwa utaguswa na kubarikiwa, Bwana Yesu asifiwe!

Download Audio

Social Media
Facebook: Kome Udu
Instagram: @udukome
Twittter: @udukome Email: iamkomeudu@gmail.com
Youtube: iamKomeUdu Website: www.iamkome.com

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top