Connect with us

Kinachomtofautisha Goodluck na wanaotaka kuwa kama yeye ni hiki hapa!

Uncategorized

Kinachomtofautisha Goodluck na wanaotaka kuwa kama yeye ni hiki hapa!

Kumekuwepo na wimbi kubwa la waimbaji wa muziki wa Injili hapa Tanzania mbao wamejitokeza kipindi ambacho Staa mpya wa muziki huu wa Injili Goodluck Gozbert alipo toa albamu yake ya pili iitwayo IPO SIKU kitu ambacho kimewafanya vijana wengi wajitokeze na kufanya muziki huu jambo ambalo ni jema na zuri sana na linapaswa kupongezwa na kila mtu na mpenda maendeleo ya muziki wa Injili hapa nyumbani.

Goodluck Gozbert akifanya uzinduzi wa album yake ya IPO SIKU katika ukumbi wa kanisa la CCC upanga jijini Dar es salaam.

Vijana hawa kwa nyakati tofauti ukikutana nao na kufanya nao mazungumzo kila mmoja wao kati ya watatu lazima amtaje mwimbaji Goodluck kama kioo kwake, kuanzia kuimba, kucheza, uvaaji na wengine wameenda mbali zaidi hata mapozi yao ya picha ama waimbapo basi lazima waige vile ambavyo anafanya Goodluck Gozbert, kuiga si jambo baya ni jambo zuri kama kweli unataka kufanikiwa ama kuwa kama yeye au kumzidi huyo unayetaka kumuiga.

Goodluck Gozbert akiwa katika pozi moja ya picha aliyopiga akiwa studio.

Jambo linalonisukuma kuandika makala hii ni kumtofautisha Goodluck Gozbert na Vijana wanaosema kuwa wanamuiga, Gozbert ni mwimbaji kijana tena ni Mtanashati hasa na ndio maana pengine vijana wengi wa kiume na wakike wanavutiwa na namna ya uimbaji wake na uvaaji wake lakini hapa nawazungumzia vijana hasa wanaoimba muziki wa Injili, ambao wanasema wanamuiga Goodluck wamejikuta wakipokelewa kwa sura ya tofauti na jamii ya kilokole(Wapendwa) kwa kufananishwa na watu wasiotambua majira na nyakati, vijana hawa wamejikuta wakiingia na masweta, jakets, kofia hata cheni makanisani kutaka kuhudumu kwenye Madhabahu ambazo watu huwa wanapeleka shida zao kwa Mungu, Kuvaa vitu ambavyo nimeviainisha hapo juu sio dhambi ila una vaa sehemu husika?

Vijana wengi hasa waimbaji wamejikuta wakitumia jasho na nguvu nyingi kutafuta jina kwa kila aina ya namna wazijuazo wao wenyewe na kujikuta wakikata tamaa baada ya kuona mwenzao akiendelea huku kukiwa hakuna maswali mengi juu yake kama yalivyo kwao, Tatizo kubwa liliopo kwa Vijana hawa ni kushindwa kujua namna ya kwenda na upepo nikimaanisha majira na nyakati ya namna ya kusoma watu kwa kipindi hicho wanataka nini au kitu gani?

Goodluck Gozbert akiwa anaimba katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Ukimtazama Goodluck Gozbert hasa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii unaweza kuona anavaa kila aina ya nguo ambayo anaona kwake ni nzuri na inampendeza, lakini hutamuona amevaa nguo za kupigia picha akaingia nazo Kanisani, Goodluck Gozbert ana mavazi yanayoendana na eneo husika, akiwa anafahamu anahudumu au kuimba kanisani tena kwenye ibada ya kawaida utamuona anavaa nguo za ibadani, kama ataimba kwenye Tamasha ambalo linafanyika Kanisani basi atavaa kuendana na ibada ya tamasha maana tu linafanyika kanisani, lakini anapokuwa anaimba kwenye viwanja vya wazi kama uwanja wa Taifa, Mlimani City n.k Pia kuna mavazi ambayo atayavaa kulingana na eneo husika maana kwenye viwanja kama hivyo huwa wanakuja watu tofauti tofauti na si wapendwa pekee, jambo ambalo halifanyiki kwa vijana ambao wanasema wanataka kuwa kama Goodkuck hapo ndipo mwenzao anapowafunga goli ambalo halina kipa, wao wanajikuta wakivaa mavazi sehemu ambayo haiendani na eneo husika, nguo za kuvaa kwenye matamasha ya wazi wao wanazivaa kwenye Ibada, nguo za kupigia picha wao wanataka wakaimbie kwenye matamasha jambo ambalo wanayemuita ni kiongozi wao yeye hafanyi hivyo, pengine anaweza akawa anaona nguvu kubwa inayotumika kumfikia ila wanashindwa kufikia kwa sababu ya makosa madogo madogo ambayo kama wataaamua kuyarekebisha basi watakuwa waimbaji wazuri sana kwa jamii na pengine wakamfikia ama kumpita kabisa.

Jambo la kuzingatia hapa ambalo waimbaji wengi hawalifahamu hasa vijana wa sasa ni kutofautisha  mavazi na sehemu za kuimbia nini kinahitajika na wakati gani huwezi ukaenda Tabora umevaa Cheni ama mkoa wowote halafu watu wakakuita wewe ni mtumishi, watakuona kama mhuni na pengine ukajikosesha na mialiko mingine kwa watumishi wengine ambao walipenda wimbo wako ila kutokana na namna ya uvaaji wako ukajikosesha fursa za mialiko ambayo kwa waimbaji wengi ni baraka na ndiyo ambayo huwa inawanufaisha waimbaji wengi na lazima ifahamike kuwa raha ya kuimba upate mialiko na hasa ya nje na unapotoka inakufanya ufahamike kwa haraka na kukuza soko la huduma yako ya uimbaji.

Ushauri wangu kwa Vijana wanaokuja na Sera ya Ugoodluck basi wajitahidi kwendana na mwenye sera mwenyewe GoodluckGozbert kwa matendo wasiseme wanafuata sera ya Ugoodluck kumbe wanafanya sera zao wenyewe ni kheri basi ufanye mwenyewe na usiseme unataka kuwa kama fulani wakati huendani na sera zake na hili ni ombi langu kwa vijana waimbaji mjitahidi kuvaa nguo kuendana na eneo husika ili msifanyike makwazo kwa watu ambao mnataka kuwahudumia isijie ikatokea umepanda mahali ili uwahudumie watu ukajikuta wewe ndio wanakuhudumia hii ilishawahi kutokea miaka ya 2007 kuna moja ya kundi maarufu lilijizolea umaarufu mkubwa walipatiwa mwaliko wakuimba walipopanda jukwaani baada ya kuwahudumia watu wakajikuta wao ndio wanahudumiwa na mpaka leo hii hilo kundi halijaweza kusimama tena.

Kama mwimbaji umepewa mwaliko jambo la kwanza kuuliza hata kabla ya kufanya taratibu zingine uliza kwanza Tukio husika linafanyika wapi? kanisani, viwanjani, ukumbini na hata kama ni viwanja pia vimegawanyika katika makundi mawili la kwanza ni viwanja ambavyo huwa vinawaleta watu wa aina zote kama National Stadiums(viwanja vya taifa) kama vile uwanja wa Uhuru, CCM Kirumba, Nangwanda-Mtwara, Karurta na Karume na viwanja vya kundi la pili ni vya shule na vyuo, ukishajiridhisha na mahali ambapo utakwenda kuhudumu basi utakuwa na uwanja mpana zaidi wa kufahamu uvae vazi gani kutokana na mahali husika na hutajikuta unafanyika makwazo na badala yake utajikuta umekuwa baraka kubwa na fursa nyingi ikiwemo mialiko itamiminika kwako sababu kubwa tu umetambua ufanye nini na kwa wakati upi.

Kwa ushauri , maswali wasiliana na mwandishi wa makala hii Johnson Jackson(Balozi wa vijana Tanzania) kupitia:

Simu: +255 655 334 949
Whatsapp: +255 653 231 198
Facebook: Johnson Jackson
Page Facebbok: Balozi wa Vijana Tz
Instagram: @Johnson Jackson63
YouTube: Johnson Jackson
Email: johnsonjackson32@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

More in Uncategorized

To Top