Connect with us

KENYA: Waumini wa Kanisa la PAG Wampiga Pasta kwa Kurefusha Ibada

Waumini wa Kanisa la PAG Wampiga Pasta kwa Kurefusha Ibada

Top Stories

KENYA: Waumini wa Kanisa la PAG Wampiga Pasta kwa Kurefusha Ibada

Vita vilizuka katika Kanisa la Pentecostal Assemblies of God-Kenya (PAG-K) eneo la Sabatia, kaunti ya Vihiga kuhusiana na ibada kuchukuwa muda mrefu kinyume na ilivyotarajiwa.

Inaripotiwa kuwa kanisa hilo limegawanyika katika makundi mawili, moja linamuegemea pasta na lingine lina kiongozi wao binafsi na jina maarufu kama “caretaker”. Makundi hayo mawili yanaabudu katika kanisa moja lakini kwa zamu, Citizen imeripoti.

Wakati wa ibada Jumapili, Novemba 21, kundi la “caretaker” linasemekana kuchukuwa muda mrefu kuabudu kinyume na inavyotarajiwa, hatua ambayo ilimkasirisha pasta wa kundi lililokuwa linasubiri nje. Vita vilizuka huku kundi lililokuwa nje likivamia majengo hayo na kujaribu kuwafukuza waumini wa kundi la “caretaker”.

Wakati wa kisa hicho, mwanamke mmoja alipigwa kichwani na chuma ambayo hutumika kupiga kengele kanisani huku nguo za pasta zikiraruliwa. Polisi kutoka Lunyerere waliingilia kati na kutuliza hali hiyo huku watu watatu wakipata majeraha.

Chanzo: TUKO

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top