Connect with us

Kenya: Mfanyabiashara Aliyebomoa Kanisa Kufungwa Jela kwa Kudharau Mahakama

Mfanyabiashara Aliyebomoa Kanisa Kufungwa Jela kwa Kudharau Mahakama

Top Stories

Kenya: Mfanyabiashara Aliyebomoa Kanisa Kufungwa Jela kwa Kudharau Mahakama

Mfanyabiashara anayekabiliwa na mashtaka ya kubomoa kanisa kinyume cha agizo la mahakama kuu, anakumbana na hatari ya kufungwa jela.

Hussein Adan Somo anaripotiwa kubomoa Kanisa la Wings of Life Gospel Church International Trustees licha ya Mahakama Kuu ya Milimani kutoa agizo ya kuzuia kubomolewa kwa kanisa hilo mnamo Aprili 23 2021. Kwa mujibu wa mtandao wa habari Taifa Leo.

Askofu Mkuu wa kanisa hilo Gerishon Njoroge alimuomba Jaji Samson Okong’o amwadhibu vikali Somo ili iwe funzo kwa watu walio na tabia ya kukaidi amri za korti. “Naomba hii mahakama imwadhibu vikali Somo kwa vile alibomoa Kanisa ilhali kulikuwa na agizo asilibomoe,” alisema Njoroge.

Mahakama ilifahamishwa kuwa kanisa hilo lilipata hasara kubwa ya zaidi ya KSh150milioni baada ya matingatinga ya Adan Somo kubomoa majengo yote. Majengo hayo ni ikiwemo chuo cha Bibilia, kanisa, na shule ya chekechea. Katika kisa hicho cha Aprili 23,2021, wahuni zaidi ya 300 na maafisa wa polisi 40 ndio waliosimamia ubomozi huo huku Njoroge akifukuzwa kwa mapanga. Njoroge alieleza mahakama kuwa alipewa kipande hicho cha ardhi na lililokuwa baraza la jiji la Nairobi mwaka 1991 na kisha kupewa cheti cha umiliki mwaka 1997. Kando na kubomoa kanisa lake Njoroge, Adan Somo pia alibomoa kanisa lingine akidai ardhi yote iliyojengwa makanisa hayo ni yake.

Akijitetea, Adan Somo alishikilia kuwa ardhi hiyo ni yake na imenyakuliwa na kugawanyishwa vipande vinne. Aliomba mahakama msamaha na kusema kuwa yuko tayari kuwaruhusu Wakristo kuingia katika ploti hiyo kusali. Uamuzi wa iwapo atafungwa jela utatolewa Desemba 15, 2021.

Chanzo: TUKO

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top