Audio: Kenny Polz - Tawala - Gospo Media
Connect with us

Audio: Kenny Polz – Tawala

Audio

Audio: Kenny Polz – Tawala

Baada ya kufanya vizuri kupitia wimbo wake uitwao Anafanya aliouachia mwaka 2017 mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili Kenny Polz, akiwa moja kati ya mwimbaji anayendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania, Na leo ameachia wimbo wake mpya uitwao Tawala ukiwa ni wimbo wake wa kwanza katika mwaka 2018, ukiwa umetaayaarishwa ndani ya studio za G Records chini ya mikono ya prodyuza KGT Shadeed.

Katika maisha yetu leo mara nyingi tumekuwa tukitumia akili zetu za kibinadamu kuongoza na kutawala mambo yetu na kila kitu katika maisha yetu na kusahau kwamba mfalme na mmiliki wa vyote tunavyoviona ni Bwana Yesu pekee hivyo yatupasa kumruhusu yeye aingie ndani ya mioyo yetu na kuyaongoza maisha yetu kwa maana kwa uwezo wetu na akili zetu hatuwezi kutenda sawa na mapenzi yake.

Tawala ni wimbo unaotukumbusha juu kumtegemea Mungu katika kila jambo linalogusa maisha yetu kwakuwa yeye ndiye kila kitu duniani na mbinguni, wimbo huu ukuguse na umruhusu Yesu sasa aingie ndani yako na atawale na kuongoza maisha yako, Ameen.

Kenny Polz ni moja kati ya waimbaji mwenye kiu ya kumtumikia Mungu na kuwahudumia watu kupitia muziki wa Injili ambao anaamini kuwa ni muziki wenye nguvu zaidi duniani katika kugusa na kubadilisha maisha ya watu wengi.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye nguvu ya kubadilisha maisha yako na hakika Yesu atakwenda kutawala maisha yako kuanzia sasa, Barikiwa.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Kenny Polz kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 672 855 256
Facebook: Kenny Polz
Instagram: @kennypolz  YouTube: Kenny Polz

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top