Videos

Music Video | Audio: Kennedy Gerald – Ninaongozwa

Kutoka jijini Dar es salaama Tanzania leo kwa mara ya kwanza nakukaribisha kutazama video ya kipekee iitwayo Ninaongozwa kutoka kwa muimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Kennedy Gerald, video ya wimbo huu imeongozwa na director Jackson Joachim kutoka Blessing Studios na muziki ukiwa umetayaaishwa na prodyuza Innocent Mujwahuki kutoka studio za Push Up Records.

Akizungumzia kuhusu wimbo huu muimbaji Kennedy Gerald amesema:-

”Neno linasema mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe, kwa hiyo wimbo wa Ninaongozwa umebeba maana hiyo kwamba bila kuongozwa na Bwana hatuwezi kwenda, bila kuongozwa na Kristo hatuwezi kufika popote, katika njia zetu tumkiri yeye naye atafanya.

Najua kuna vitu vingi tunafanya katika maisha yetu lakini tukumbuke pia tuna safari ya kwenda mbinguni kwa hiyo bila kuongozwa na Kristo na kulitii neno lake hatuwezi kufika salama na huu ndio ujumbe halisi ulibebwa katika wimbo huu. Mungu ambariki yeyote atakayesikiliza na kupokea neno la Mungu kupitia wimbo huu, Ameen.

Kwasasa ninaishi Dar es salaam nikiwa ni mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye nimeokoka na naabudu katika kanisa la Pentecost, Tabata kisiwani kwa Pastor John Shusho. Nina album moja ikiwa kwenye mfumo wa audio CD iitwayo Elshadai na video ambayo nimeachia kwasasa ni ya wimbo huu uitwao ‘Ninaongozwa’.” – Alimaliza muimbaji Kennedy Gerald.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii yenye habari njema na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukupa nguvu ya kubadilisha mawazo na akili zako na kumtegemea Yesu Kristo katika kila jambo lako. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na muimbaji Kennedy Gerald kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 769 823 566
Facebook: Kennedy Gerald
Instagram: @kenny_gerald
Twitter: @kennygerald
Youtube: KennedyGerald

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Video | Music Audio: Sound Special Gospel Singers - Merry Christmas & Happy New Year

Next post

Music Video | Audio: Okito Feat. Alain - Amenipa Nafasi