Music

Audio: Judith Mbilinyi – Jina la Yesu

Mara baada ya kufanya vizuri mwaka 2016 kupitia wimbo wake mzuri wa kuabudu uitwao Maisha Yangu kwa mara nyingine tena muimbaji wa nyimbo za Injili aliyebarikiwa sauti ya pekee anayefahamika kwa jina la Judith Mbilinyi ameachia tena wimbo wake mzuri uitwao Jina la Yesu, muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Epignosis chini ya mikono ya prodyuza Malima.

Akizungumza na gospomedia.com muimbaji Judith Mbilinyi alisema machache kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu:-

”Ninamshukuru Mungu aliye achilia neema na kibali cha kuuhifadhi wimbo huu kupitia sauti (audio). Natamka uponyaji, kuhuishwa, kurejeshwa kwa vile vitu na mambo ambayo adui alikua ameiba kwenye maisha yako, kadiri unavyoendelea kusikiliza wimbo huu ndivyo Mungu anaendelea kushugulika na maisha yako.” – Judith Mbilinyi

1 Wakorinto 1:18
Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.”

Kwa moyo wa unyenyekevu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utakwenda kukubariki katika viwango vingine vya tofauti kabisa. Barikiwa!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Judith Mbilinyi kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 762 372 408
Facebook: Judith Mbilinyi
Instagram: @judithmbilinyi
Youtube: Judith Mbilinyi

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio: Nehemia Kindole - Wema na Fadhili

Next post

Video | Audio: Florence Andenyi - Mungu wa Miungu