Audio: Judia - Amenitengeneza - Gospo Media
Connect with us

Audio: Judia – Amenitengeneza

Audio

Audio: Judia – Amenitengeneza

Baada ya kufanya vizuri sana kupitia video ya wimbo wake uitwao Ni Neema mwimbaji mpya anayezidi kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania Judia Amisi ameachia wimbo wake mpya uitwao “Amenitengeneza” ikiwa ni wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2018, Ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Still Alive zilizopo jijini Nairobi nchini Kenya.

“Yakobo 1: 2-3 Jaribu linapo kujia bila shaka Mungu anakuwa anakutengeneza kwa ajili ya mazuri yajayo, Amekushindia mengi sababu amekuumba kushinda na si kushindwa… Kukata tamaa wala woga si vyako tena maana amesema “TUSIOGOPE” hivyo usiogope, na kwamba yote uliyokutana nayo mpaka uifikie siku ya leo alikuwa tu “Anakutengeneza “. Na sababu Tumetengenezwa tuimbe wimbo wangu huu mpya “AMENITENGENEZA ” na BWANA akubariki. Petro 5:10. ” –  alisema Judia

Nina imani kuwa kupitia wimbo huu utapata kubarikiwa na kuinuliwa kwenye viwango vingine vy kiroho, kiafya, kiuchumi, mahusiano, ndoa, ajira na vyote ambavyo vimekuwa ni kikwazo kwako, Tambua Bwana Anakutengeneza, Mungu Amekutengeneza, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Judia Amisi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255624068127
Facebook: Judia Amisi
Instagram: @judia9
Snapchat: Judia99
Youtube: Judia Amisi

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top