Connect with us

Josiah Justice Yupo Tayari Kwa Ujio Wake Mpya. Awaonya Waimbaji.

Habari

Josiah Justice Yupo Tayari Kwa Ujio Wake Mpya. Awaonya Waimbaji.

Mwimbaji wa nyimbo Injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania Josiah Justice ameweka wazi kuhusu ujio wa wake mpya anaotarajia kuuachia hivi karibuni.

Mwimbaji Josiah Justice ambaye kwasasa ameachia nyimbo tatu zinazofanya vyema katika tasnia ya muziki wa Injili ikiwemo ile ya ”Asingekuja Yesu”, ”Naomba Unipe Nguvu” na ”Ni wewe Uliyetenda” ambazo zote zimekuwa baraka kwa watu wengi kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Akiongea na timu ya habari ya gospomedia.com mwimbaji Josiah Justice amesema kuwa kwa sasa yupo ndani ya studio za Relights akifanya maandalizi ya wimbo mwingine mpya ambao upo mbioni kuachiwa ukiwa umetayaarishwa na prodyua Ivan.

Josiah Justice ambaye kwasasa anatumika kihuduma katika kanisa la EAGT JESUS Village amesema kuwa wimbo huo mpya utakuwa ni wa baraka zaidi kwakuwa anaamini utakwenda kugusa roho na nafsi za watu wengi zaidi ambao watapa badiliko la kiroho kupitia kazi hii,  Hata hivyo amezungumzia changamoto mbalimbali alizoziona katika kiwanda cha muziki wa injili hasa Tanzania kuwa waimbaji wengi wa siku hizi wamesahau lengo zima la muziki wa injili na kuweka maslahi mbele na kusahau kutunga nyimbo zenye ujumbe mzuri kulingana na Mungu alivyo wajalia na kuwaongoza na kuwasihi waimbaji kurudi katika kusudi la Mungu ili Injili iweze kuenea mjini na vijijini.

”Waimbaji wengi hupenda kuiga nyimbo za wenzao au kuchukua mziki wa kidunia na kubadili maneno tu kitu ambacho si sahihi hasa kwa watoto wa Kristo, silaha kubwa ya kumshinda shetani katika hili ni kuwa karibu na Mungu kwakuwa yeye hukaa katikati ya sifa”. Alisema Josia Justice.
Kama bado hujapata nafasi ya kusikiliza wimbo wa ”Asingekuja Yesu” Tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua. Karibu!!

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Josiah Justice kupitia
Simu/WhatsApp: +255 714 390 059
Facebook: Josiah Justice255
Instagram: @josiahjustice
Twitter: josiahjustice_
Email: Josiah@josiahjustice.com
Website: https://josiahjustice.com/

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top