Audio: Joseph Misa Feat. Prince Denic - King'amuzi - Gospo Media
Connect with us

Audio: Joseph Misa Feat. Prince Denic – King’amuzi

Audio

Audio: Joseph Misa Feat. Prince Denic – King’amuzi

Kutoka mjini Moshi kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya katika huduma ya muziki nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Joseph Misa na huu ni wimbo wake mpya kuachia uitwao King’amuzi akiwa amemshirikisha mwimbaji Prince Denic.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Kim’s Records chini ya mikono ya prodyuza Geofrey Fedrick.

“KING’AMUZI ni wimbo unaogusia sana mtindo wa hali ya maisha ya sasa na jinsi watu walivyo sahau njia ya Mungu na kufuata mienendo ya dunia hii.
Dunia ya sasa imekuwa kama hakimu kwa kuhukumu kila kifanyikacho na wengi, Wengi wamejifanya Ving’amuzi kwa kusambaza Habari zisizokuwa na ukweli wowote huku wakisababisha chuki na mafarakano katika familia.

Kikubwa ni kwamba uonapo mwenzako yupo katika wakati mgumu au majaribu chukua jukumu la kumuombea na sio kuzurura mitaani ukitoa habari za unafiki na uongo.

Kazi ya Mungu tumwachie Mungu na tukiri kwamba Yesu alitufia Msalabani na tumrudi yeye kwa mioyo yetu yote, Barikiwa kila usikilizapo wimbo huu na mwenyezi Mungu akuongoze katika nyayo za njia inayostahili mbele zake.” – alisema Joseph Misa

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri tukiamini kuwa utakugusa kwa namna ya kipekee, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasilianA zaidi na mialiko ya kihuduma watiliana na mwimbaji Joseph Misa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 744 162 727
Facebook: Joseph Misa
Youtube: Joseph Misa

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top