JOHN PAZIA: BIFU NI SUMU KWENYE MUZIKI WA "GOSPO". - Gospo Media
Connect with us

JOHN PAZIA: BIFU NI SUMU KWENYE MUZIKI WA “GOSPO”.

Habari

JOHN PAZIA: BIFU NI SUMU KWENYE MUZIKI WA “GOSPO”.

Mwanahabari na mdau wa muziki wa Injili toka jijini Arusha,John Pazia amewataka waimbaji
wa muziki wa injili na watumishi kwa pamoja kuwa na ushirikiano ili kuwezesha tasnia hiyo kufika
mbali na kuacha na chokochoko ambazo mara zote zote hazijengi.
Akiongea na Gospomuziki.Com,Pazia amesema,”bifu sio kitu kizuri kabisa na halitakuwi kuonekana kwa watumishi wa Mungu sababu bifu huondoa ushirikiani ,upendo na kusaidiana na wenzako
katika maisha ya kila siku na ya kihuduma.Bifu hizi zinakuja kutokana na kujiona wewe ni bora
zaidi ya mwenzako kitu ambacho ni sumu kwenye huduma,kama waimbaji tunataka kuona huduma
hii inapiga hatua kubwa ni lazima mabifu yasiyo na maana yaishe ,kama waimbaji wa bongo
fleva wanasamehana na wanafanya kazi pamoja sembuse sisi wana wa Mungu na tena maandiko matakifu yametuonya kuwa mambo haya yasitajwe kwenu,ni wakati wa kumaliza tofauti zozote
bila kujali ukubwa wa tofauti hiyo bali ni kusamehe na kushirikiana ili injili iwafikie wasiofikiwa”
Reported By: Douglas Kyungai
Ripota wa GospoMuziki,ukanda wa kaskazini

More in Habari

To Top