Music

Audio: Joel Masingisa – Wastahili (You Deserve)

Baada ya wiki chache kuachia wimbo wake mzuri wa kuabudu uitwao ”Ndani Yako” ikiwa ni moja ya nyimbo inayoendelea kufanya vizuri katika tovuti hii pendwa ya kikristo Tanzania, leo kwa mara nyingine tena mwimbaji Joel Masingisa ameachia wimbo wake mwingine wenye kugusa nafsi uitwao Wastahili(You Deserve) muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Rachel Records chini ya mikono ya prodyuza Michael Robert.

”Kuna kiwango cha maisha upo kwasasa na ukitafakari kwa makini unaona si kwa uwezo wako bali ni kwa Neema tu…., Kuna kazi nzuri unaifanya na ukitafakari unaona si kwa uwezo wako bali ni kwa Neema tu.., kuna biashara nzuri unaifanya na inakulipa vizuri ukitafakari unaona si kwa nguvu zako bali ni Neema tu…., Kuna kiwango kizuri cha elimu umekifikia na ukitafakari kwa kina umefikaje hauna majibu kwakuwa ni Neema tu.. Basi inua moyo wako Mwambie Mungu WASTAHILI…. Mwambie Bwana Yesu WASTAHILI TU.. Isaya 54:14 – Utathibitika katika haki na utakuwa mbali na kuonewa…Wimbo huu unagusa maisha yangu na unagusa maisha yako karibu tutafakari kwa pamoja. – Alisema mwimbaji Joel Masingisa

Nina hakika kuwa wimbo huu utakwenda kukupa utafakari mpya katika matendo makuu aliyoyafanya Mungu katika maisha yako, hakika Bwana WASTAHILI, Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Joel Masingisa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 742 971 209
Facebook: Joel Masingisa
Instagram: @masingisajoel
Youtube: Joel Masingisa

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Video | Audio: Yohana Mpangule - Nibariki

Next post

Video | Audio: Moji Short Babaa, Gurdian Angel, DK Kwenye Beat - Hajawahi Niangusha