Audio

Audio: Joel Masingisa – Ndani Yako

Kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayefahamika kwa jina la Joel Masingisa akitokea mjini Moshi Kilimanjaro, leo kwa mara ya kwanza anakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo wake mzuri wenye mahadhi ya kuabudu uitwao Ndani Yako muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Michael Robert kutoka ndani ya studio za Rachel Records.

Akizungumzia kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu muimbaji Joel Masingisa alikuwa na haya ya kusema:-

”Ujumbe wa wimbo huu niliupata kwenye kitabu cha Matendo 17:28 ambao unasema kwamba ”Ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu….. Yako Mambo mengi…. Yametusonga na kutufanya tuishi maisha ya mashaka na shida….Yametufanya kujiona dhaifu na mioyo kuinama…Kila unalolifanya haliendi….Lakini Ni saa ya Kukaa na Bwana….Maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda na Kuwa na uhai wetu Ameen!. huu ni wimbo unaogusa Maisha yangu.” – Alisema muimbaji Joel Masingisa

Nina imani kuwa utabarikiwa na wimbo huu ambao utaweza kuhamisha akili yako na roho yako katika sura nyingine ya kumuabudu Mungu na kupata nguvu mpya ya matumaini. Barikiwa!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Joel Masingisa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 742 971 209
Facebook: Joel Masingisa
Instagram: @masingisajoel
Youtube: Joel Masingisa

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: James Ezekiel(The God Son) Feat. Joshua Laizer - Niumbie Moyo Safi

Next post

Audio: Elvis Kiwanga - Showers of Blessings