Video | Audio: Joel King - Yesu Tumaini - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Joel King – Yesu Tumaini

Audio

Video | Audio: Joel King – Yesu Tumaini

Mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili akitokea jijini Dar es salaam Tanzania Joel King ameachia video ya wimbo wake uitwao “Yesu Tumaini” video ikiwa imeongozwa na director Debro na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Faith Music Lab.

Huu ni wimbo uliobeba ujumbe wa sifa na maombi ya kukiri kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu kwakuwa yeye ndiyo tegemeo letu, tumaini letu na kimbilio letu kila iitwapo leo leo Yesu ni tumaini la pekee.

Yesu Tumaini la pekee ni wimbo unaobeba jina la albamu yake ya kwanza yenye mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwa katika mfumo wa Audio CD na Video na DVD inayotarajiwa kuachiwa rasmi mapema mwaka huu 2018.

Ni hakika utabarikiwa na kuinuliwa baada ya kuitazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni imani na matumaini yangu kuwa utakugusa kwa namna ya kipekee sana, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Joel King kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 659 800 602
Facebook: Joel King
Instagram: @joelking

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top